Octoba 14
mwaka huu Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza zitamenyana timu za Toto Africa
pamoja na timu ya Pamba sc zote za jijini Mwanza, timu hizo kwa sasa ziko ligi
daraja la kwanza kundi C ambapo mpaka sasa kila timu imecheza jumla ya michezo
4 ambapo Toto African wao wanajumla ya pointi 4 huku Pamba sports Club wao
wakiwa na jumla ya pointi 2 na kushika mkia katika kundi C. Kuelekea mchezo huo
championi limekuletea baadhi ya mambyoa mabyo huenda yatatokea katika mchezo
huo.
PAMBA KUTUMIA UKONGWE.
Mara zote
kuelekea katika mchezo unazokutanisha timu ya Toro African na Pamba sc mchezo
huu huwa mgumu kutokana na historia ya timu hizi mbili, kwanza Klabu ya soka ya
Pamba ndiyo klabu kongwe kuliko timu ya Toto African ambapo Pamba imeanzishwa
mwaka 1968 mbele ya Uwanja wa CCM Kirumba huku Toto African yenyewe ikianzishwa
mwaka 1972 hivyo kutokana na Ukongwe huo Pamba sc inapewa nafasi ya kuweza
kuushinda mchezo huo lakini wachambuzi wa maswala ya soka wanasisitiza kusubiri
dakika 90 ziweze kuamua.
Rekodi zinambeba Pamba SC
Klabu ya
soka ya Pamba sc ambayo ilianzishwa mwaka 1968 imewahi kutwaa Ubingwa wa ligi
kuu bara mwaka 1990 enzi hizo ligi daraja la kwanza lakini pia mwaka 1989 na mwaka 1992 timu hiyo
pia ilitwaa Ubingwa wa michuano ya Nyerere Cup ambapo Pamba fc ilipata nafasi
ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa kabla ya kushuka daraja rasmi
mwaka 2000 ambapo haijapanda daraja mpaka leo hivyo Pamba kama ikitumia uzoefu
wake katika mashindano huenda ikapata pointi katika mchezo huo ambao utakuwa
mkali na wa aina yake kwa timu zote mbili kutokana na historia iliyopo.
Toto African Panda shuka
Klabu ya
Toto African ni miongoni mwa timu zeye bahati na ligi kuu bara lakini baadhi ya
wadau wake wasioitakia mema wamekuwa wakiishusha daraja lakini pia kitendo cha
timu hiyo kuwa katika ligi kuu bara na
kupania mchezo wake na Simba huwa kinawakera wadau wengi wa soka jambo
linaloifanya timu hiyo ishindwe kujitengenezea mazingira ya kusalia kwenye ligi
na tangu timu ya Pamba sports Club ishuke daraja Toto African imecheza ligi kuu
bara ikipanda daraja na kushuka kwa zaidi ya misimu mitatu hivyo kutokana na
Toto African kuwa na uzoefu mkubwa katika ligi hiyo inaweza kupata matokeo katika mchezo huo
japokuwa soka la timu hizi mbili huwa halitabiriki.
Rekodi ya timu hizo zilipokutana.
Kwa mujibu
wa aliyekuwa Kocha mkuu wa timu ya Pamba Venance Kazungu ambaye amehudumu
katika timu hiyo kwa muda mrefu ameliambia gazeti hili kwamba katika michezo
mingi ambayo timu za Toto African na Pamba , Klabu ya Pamba imekuwa ikipata
matokeo mara nyingi zaidi kuliko pamba ambapo katika msimu wa mwaka 2013/14
timu hizo zilipokuwa ligi daraja la kwanza kundi C timu hizo zilikunata septemba 14 ,2013 timu ya
Toto African ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lakini pia timu hizo
ziliporudiana sebruari 22 mwaka 2014 timu ya Pamba iliibuka na ushindi wa bao
1-0 na msimu wa mwaka 2016/17 timu hizo zilikutana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
katika mchezo wa kombe la FA na Toto iliifunga Pamba bao 4-1 hivyo mchezo wa
timu hizo utakuwa mkali na wakusisimua.
Toto African vs Pamba derby ya tatu
Tanzania
Ukiachana na
Derby ya Simba na Yanga ambayo ndiyo derby ya tatu barani Africa baada ya ile ya nchini Misri ya Al ahly vs
zamaleck na Orlando Pirates vs KaizerChiefs ya Afrika kusini , katika nchi yetu Derby ya pili ni ile ya
African Sports dhidi ya Coastal Unioni na derby ya tatu ni Pamba dhidi ya Toto
African hivyo kutokana na ukumbwa huo mchezo wa timu hizo utakaopigwa Otoba 14
mwaka huu Uwanja wa Nyamagana jijini hapa utakuwa na ushindani wa aina yake.
Vikosi vya timu zote mbili.
Kuelekea
mchezo wa timu za Pamba dhidi ya Toto African vikosi vyote viko katika hali
nzuri kwani timu hizi zinaelekea katika mchezo huo huku Toto African wakiwa na
jumla ya pointi 4 huku Pamba sc wao wakiw ana pointi 2 pekee baada ya michezo 4
hivyo kikosi kitakachojiandaa vizuri ndicho kitakachopata matokeo kwani timu
hizi huwa hazikutani mara kwa mara na badala yake kukutana kwake mpaka matukio
maalumu kama hivi ligi daraja la kwanza.
Mashabiki wa timu zote mbili.
Mpaka sasa
timu ya soka ya Pamba ambayo iliwahi kutamba hapo nyuma katika soka la nchi hii
imewapoteza mashabiki wake baada ya kuanza vibaya michuano hii ya ligi daraja
la kwanza hivyo endapo itafanya vizuri katika mchezo wake a Toto, itaendelea
kukuza mtaji wake wa mashabiki lakini pia Toto African nao wakipata ushindi
wataendelea kuw ana mtaji wa mashabiki waliokuwa nao kwani timu hiyo imeshinda
mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mmoja huku ikipoteza michezo 2 hivyo timu
yoyote itakayofungwa katika mchezo huo itakuwa imepoteza ramani ya kufanya vema
katika ligi daraja la kwanza ikiwa ni pamoja na kupanda daraja kuelekea ligi
kuu.