Na Johnson James, Mwanza
Samson
William Noah maarufu kama Jet man ni
kijana mwenye kipaji cha sanaa aliyezaliwa wilayani Ilemela jijini Mwanza
maeneo ya Nyasaka Msumbiji na alikuwa na
ndoto lukuki za kufanikiwa katika maisha yake, ghfla mwaka 2011 ndoto zake
zilikata baada ya kupata hitlafu ya mgongo hali ambayo ilipelekea kulala
kitandani tokea mwaka huo mpaka leo hii,
Jetman ni moja kati ya wasanii ambao walikuwa wakifanya vema katika muziki wa
Danso na Ragger, Mwanza music Housen imefanya mahojiano maalumu kufahamu nini
tatizo limepelekea yeye kulala kitandani kwa zaidi ya miaka 5 sasa bila kuwa
na uwezo wa kukaa wala kusimama.
Unasumbuliwa na nini haswa?
"
kikubwa kinachonisumbua zaidi spine code yaan
ni uti wa mgongo na sehemu ambayo imepata shida ni kiuno kwani kuna
sehemu kiunoni haipo mahala pake hivyo siwezi kufanya lolote kwani hiyo sehemu
ikishtuka hubana mishipa ya fahamu na kupelekea
miguu kufa ganzi kwa muda mrefu sana na kukosekana kwa mawasiliano kati
ya kiuno na miguu" alisema
Tatizo lilianza lini na lilianzaje?
tatizo
limeanza mwezi octoba 2011 ambapo nilikuwa kwenye pikipiki usiku nikitoka
kwenye mihangaiko , tulikuwa tunatembea kwenye lami lakini badae tukaingia
barabara ya vumbi kutokana na kuwa dereva pikipiki alikuwa mwendo kiasi
akakutana na tuta ambalo wananchi waliweka ili kuzuia ajali maeneo hayo basi
pikipiki iliruka na mimi nikaruka kwa juu nilipotua nikatua kwenye vyuma vya
pikipiki mwisho kabisa nikasikia kama kuna kitu kimevunjika kiunoni lakini
sikujali nikaenda nyumbani nikahisi nimepata tatizo kwakua maumivu hayakuwa
mengi sikujali,baada ya hapo sikupata maumivu sana lakini baada ya kama wiki
mbili nimekaa ofisini kwangu ulipofika muda wa kwenda kutafuta chakula ghafla
nikahisi miguu haina mawasiliano na kiuno nilipojaribu kuinuna nilianguka chini
tangu siku hiyo sijawahi kuinuka wala kukaa tena mpaka leo hii kumbe katika
ajali ile nilipata tatizo kubwa sana katika mwili wangu"
Unapata maumivu kiasi gani
"
nashindwa hata jinsi ya kusimulia kuhusu
tabu ninayopata lakini kiufupi napata maumivu makubwa sana ambayo kwa hakika
nikipona ntamshukuru Mungu kwani siwezi kueleza kabisa kwani maumivu ni makali
sana.
changamoto zipi unazopitia katika
ugonjwa huu
"
kiukweli napata changamoto nyingi sana katika ugonjwa huu kwani hapa nilipo
siwezi kukaa, nakojoa kwenye kopo, najisaidia kwenye ndoo kiukweli napata shida
sana na namuomba Mungu nifanikiwe hata kupata matibabu niachanane na changamoto
hizi ambazo kiukweli Mungu ndiye anajua"
Familia yako
inakusaidiaje
"
kiukweli familia yangu wananisaidia kadri ya uwezo wao mpaka leo naishi, kwanza
familia yangu haina uwezo wowote kwani ningeshapelekwa hospitali lakini
kutokana na umaskini na uwezo wa familia zetu kuwa mdogo ndiyo maana mpaka sasa
sijaenda hospitali kutokana na uwezo mdogo wa familia yangu"
Unapata msaada gani kutoka kwa wadau
wa muziki?
"
kiukweli wadau ni wadau, na tangu nipate matatizo waliokuwa marafiki zangu wote
wamenikimbia na wanaojitokeza kunisaidia
ni tofauti na wale niliotegemea hivyo nilichojifunza ni kwamba ukipata shida
marafiki wote wanakukimbia na ndivyo ilivyotokea kwangu hivyo wadau ni wachache
wanaotoa msaada kwangu katika kipindi hiki cha matatizo"
Tulisikia Mh waziri Nape na Mkuu wa
mkoa wa Mwanza walikusaidia, walikusaidiaje?
"
kwanza kabisa niwashukuru Clouds Media Group kwa kujitolea kulivalia njuga
swala hili la kuhakikisha a kuhamasisha
mimi kuchangiwa ili niweze kupata matibabu na kurudi katika hali yangu ya
kawaida , na nilipata taarifa za kusaidiwa na viongozi hawa lakini sio hao tu
kwani hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli naye
ameguswa na tatizo langu na yeye amechangia hivyo nawashukuru wote
wanaojitokeza kunichangia katika kipindi hiki" alisema
Madaktari wanakwambiaje kuhusu
ugonjwa wako
"
katika vitu vilivyonishangaza ni madaktarii wa nchi hii kwanza kama hawana
uwezo ni wagumu kukubali matatizo yao, nilipopelekwa KCMC Dar es salaam kwa ajili
ya kwenda kucheki ninatatizo gani nilipimwa kipimo kikubwa cha ajabu
nilibadilishiwa vipimo na kupewa vya mtu mwingine hali ambayo ilinishtua na
nimeamua niliseme hili kwamba kuna uzembe katika hospitai zetu lakini kwa
bahati nzuri alikuja mzungu mmoja nilipomwambia ndiye akanishughulikia na
kunipa vipimo sahihi vya kwangu hivyo katika hospitali zetu nyingi kuna huduma
mbovu"
Hali yako kiuchumi baada ya kuugua
ikoje
"
kiujumla hali yangu imeporomoka kwa asilimia zote tangu nipate matatizo kwani
ndio kwanza nilikuwa naanza kazi baada ya kutoka masomoni, kwahiyo mpaka sasa
hali yangu imerudi nyuma sana kiasi kwamba sina pakuanzia licha ya kuwa na
vipaji vya Kuchora,kudizain nguo na kutengeneza muziki niwezi kufanya lolote
kutokaa na hali yangu kwa sasa "
Vipi safari ya kwenda China
" baada ya kuona hospitali za hapa
nyumbani haziwezi kusaidia lolote kunusuru maisha yangu ili niweze kurudi
katika hali yangu ya kawaida ikanibidi
nianze kutafuta wataalamu katika hospitali za nje kupitia simu yangu ndipo
nikapata mtaalamu huko India ambaye aliahidi kufanikisha afya yangu kurudi
katika hali yake ya kawaida endapo nitafika hopitalini huko India kwahiyo hapo
ndipo zikaanza harakati za mimi kutaka kwenda India kutibiwa japo gharama ni
kubwa mno"
Vipi gharama za matibabu
"baada
ya kufanyiwa mpango wa kwenda India kupatiwa matibabu niliambia gharama za
kwenda India , kufanyiwa vipimo, na vitu vingine gharama niliambiwa shingili
milioni 22 fedha ambayo bado kwangu ni ndoto kuipata ila nina imani kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali watanisaidia niweze kupata matibabu hivyo ili
nipate matibabu mpaka nipone inanibidi niwe na fedha taslimu shilingi milioni
22 kwani kufanyiwa vipimo na matibabu ni milioni 12"
Kabla ya kuugua ngoma yako ilikuwa
ipi?
"
kwakua Mimi nilikuwa nikifanya muziki wa Ragger na Danso mpaka tatizo la mgongo
linanikuta wimbo wangu ambao ulikuwa
ukifanya vizuri ulikuwa ni My Sweet ambao niliufanyia huko Arusha ambako tatizo
lilinikuta"
Una Mke au GirlFriend baada ya kuugua
uhusiano wenu ukoje
"
Nilikuwa na girlfriend wangu ambaye tulikuwa katika mahusiano ya muda mrefu na
baada ya Mimi kuugua huu uti wa mgongo aliniacha kutokana na haya matatizo
hivyo mimi nipo tu sina uhusiano wowote kwa sasa"
Unamtoto/watoto
je wako wapi kwa sasa?
" Mimi
kwa sasa nina mtoto mmoja na niko nae nyumbani hapa Nyasaka nyumbani kwetu na
anaendelea na masomo yake licha ya Mimi Baba yake kuwa katika hali hii"
Una Ndugu? wako wapi na
wanakusaidiaje?
" Mimi
nina ndugu na wote wako Mwanza, lakini kila mmoja anauhuru na uwezo wa
kunisaidia kulingana na hali zao hivyo ndugu zangu siwezi kuwasemea kwa lolote
kwani kutoa ni moyo na sio utajiri"
Nani
anakusaidia kwa sasa
" Mimi
anayenihudumia hapa nyumbani ni Mama yangu Mzazi kwani sina mwingine wa
kunihudumia hivyo Mama yangu mzazi ndiye ananihudumia kila kitu kama Chakula,
Maji ya kunywa na mengine hivyo nampenda sana Mama yangu kwa upendo anaozidi
kunionyesha"
Ombi lako ni lipi kwa wadau na
mashabiki zao
"
Kiukweli Ombi langu kubwa kwa wadau na mashabiki wa muziki wangu ni kuwa
wajitahidi kuendelea kunichangia ili niweze kupata fedha ya matibabu kule India
ambayo kwa ujumla ni shilingi milioni 22hivyo nawaomba wadau watumie namba
0757626207 ambapo jina litakalokuja ni GODFREY KUSOLWA ambaye ndiye aliyechaguliwa
na familia kutunza mchango wote utakaotumwa hivyo naomba wadau wajitokeze
kunichangia kwa wingi ili niweze kupata matibabu"
Muziki umeufaidisha nini mpaka sasa
"
Muziki ninauheshimu sana katika maisha yangu kwani Muziki ndio umenisomesha na
umeniwezesha kuwa na fani za Uchoraji, Kudizaini nguo, na mengine mengi hivyo
kutokana na hali ya familia yangu kuwa mbaya kifedha muziki ndio ulionisaidia
kwenda Nairobi kusomea yote ahayo na nilipoanza kujipanga ili niisaidie familia
yangu ndio nikapata matatizo"
Ulikaa hospitali kwa muda gani?
baada ya
kupata hili tatizo nikiwa Arusha nilikaa katika hospitali ya Mount Meru Arusha
kwa muda wa siku tatu nikiangaliwa lakini madaktari walishindwa kugundua nina
tatizo gani ndipo nilienda hospitali ya KCMC ya Dar es salaama ambako nilikaa
kwa wiki tatu na kisha mwaka 2013 ndio nikarudi nyumbani rasimu baada ya hali
yangu kugoma kabisa huku madaktari nao wakishindwa kunaini nina tatizo
gani"
Taja nyimbo kali ambazo uliwahi
kuzitoa kabla ya kupata matatizo
" mpaka
naugua nilikuwa nimetoa jumla ya nyimbo sita huku nikiwa sijatoa albamu yoyote
licha ya nyimbo hizo sita kukamilika kuwa albamu hivyo miongoni mwa nyimbo
nilizoimba ni My Sweet, Naogopa, Nasaka mke wangu, Pozi za kichokozi, Kiuno
kiwe bize na mshike wa kwako hizi ndizo nyimbo ambazo nilitoa kabla ya kuugua"
MAMA YAKE AELEZA JINSI ANAVYOMHUDUMIA
MWANAE
Mama Mzazi
wa Samson William Noah aka Jetman
aliyejitambulisha kwa jina la Magen Malekana alipoulizwa na Championi
changamoto anazotapa kitoa huduma kwa mwanae alijibu kuwa changamoto ni nyingi
sana " Mwanangu alitoka hapa
nyumbani akiwa mzima wa Afya lakini baada ya muda nikapata taarifa amepata
matatizo hivyo najiskia vibaya mpaka sasa kwani sikutegemea mwanangu kuwa
katika hali hii ila namwachia Mungu "
unapokuwa naye mwanao amekuwa
kizungumza Maneno gani
" Mara
nyingi Mwanangu huwa anasali aweze kurudi katika hali yake ya kawaida kwani
huwa anasema " Mama hivi nitapona lini niisaidie familia yangu"
namimi huwa namtia moyo kwa kumuambia avumilie kwani Mungu ndiye muweza wa
yote" alisema
watu wamekuwa wakija kumsalimia wanao
kwa kiasi gani
"
ninachoweza kusema ni kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakija kumsalimia japokuwa
sio wengi lakini sio wengi sana na hiyo inatokana na kuwa yuko kwenye matatizo
na ninavyoona marafiki zake wengi wamemkimbia baada ya kuwa katika hali
hii"
Jetman anaishi na nani kwa sasa
" Kwa
sasa ninaishi nae katika nyumba yetu pamoja na mdogo wake hivyo ninachoweza
kusema ni kuwa niko nae nyumbani kwangu na Mimi ndiye ninamhudumia kwa siku
zote"
ombi lako kwa watanzania kwa ujumla
Ombi langu
kwa watanzania wenzangu waendele kumchangia ili aweze kupata matibabu kwani
mwangu hawezi kukaa, hawezi kusimama yeye amekuwa wa kulala miaka yote ,
tulijaribu kumnunulia baiskeli ya kutembelea alishindwa kuitumia, tukanunua na
magongo akashindwa pia kuyatumia hivyo naumia sana kuona mwanangu akiw akatika
hali hii kwahiyo naomba watanzania wamchangie mwanangu kupitia namba ya simu
aliyotaa"