Timu ya soka ya Toto african leo imemtangaza Kocha wa zamani wa Stand United, Singida United na Kemondo fc Frugence Novatus kuwa Kocha wake mkuu baada ya timu hiyo kuwa katika hatari ya kushuka daraja baada ya mpaka sasa kuwa nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi kuu bara wakia na jumla ya pointi 22 huku wakiwa wamesaliwa na mechi 7 mkononi kabla ya ligi kuu 2016/17 kumalizika
akizungumza na Championi Mwenyekiti wa Toto Africann Godwin Aiko amebainisha kuwa wameamua kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi wa timu hiyo baada ya timu hiyo kuwa katika hali mbaya " tumeongeza kocha ili timu isishuke daraja hivyo tunaamini Novatusi atafanya mengi kwa timu yetu lakini katika mabadiriko haya tuliyofanya hatujamfukuza kocha Tim Jost aliyekuwepo bali yeye atakuwa mkurugenzi wa benchi la ufundi wa timu yetu" alisema
Mwenyekiti wa Toto African Kulia akishikana mkono na Kocha mpya wa Toto african Frugence Novatus.