Mechi namba 2 Kundi C (Rhino Rangers v Alliance).
Timu
ya Alliance imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la
kutoingia vyumbani wakati wa ukaguzi na wakati wa mapumziko, kitendo
ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(13) ya Ligi Daraja la Kwanza, na
adhabu imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Daraja la
Kwanza.
Pia
viongozi wa benchi la ufundi la Alliance, Kocha Msaidizi Kessy Mziray,
Kocha wa makipa Tade Hussein, Mtunza vifaa Josephat Munge na Meneja wa
timu James Bwire wamepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kila mmoja
kwa kosa la kumbughudhi mwamuzi wakimtaka kumaliza mpira kabla ya muda
wakidai muda umekwisha wakati kazi ya kutunza muda si yao. Adhabu hiyo
ni kwa mujibu wa Kanuni ya 41(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Rhino
Rangers imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) na barua ya Onyo
kutokana na mashabiki wa timu hiyo kufanya fujo baada ya mechi
kumalizika. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja
la Kwanza.