Klabu ya soka ya Pamba sc jana ilifanikiwa kutoka sare ya kutofungana na timu ya JKT Oljoro katika mchezo wa ligi daraja la kwanza mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro, katika mchezo huo Pamba wanapaswa kujilaumu wenyewe kwani wachezaji wake walikosa nafasi nyingi za wazi ambazo kama wangefunga wangeibuka na ushindi wa pointi tatu, Mpaka sasa Pamba SC imecheza jumla ya michezo 2 imefungwa mmoja na kutoka sare mchezo mmoja lakini pia JKT Oljoro wao wamecheza michezo miwili pia na wametoka sare michezo yote , Pamba itacheza tena octoba 2 kwenye Uwanja wa Nyamagana ambapo itamenyana na timu ya Biashara fc kutoka mkoani Mara.
Aidha katika mchezo wa Pamba dhidi ya Jkt Oljoro ulishuhudia timu ya JKT oljoro wakichelewa kufika Uwanjani ambapo hapo awali mchezo huo uliokuwa uanze saa 10: 00 jioni ulichelewa kuanza kutokana na timu wenyeji kuchelewa kuingia Uwanjani ambapo waliingia Uwanjani saa 10: 15 hali iliyosababisha mchezo huo kuanza kutimua vumbi saa 10:25 jioni.
Lakini pia mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Mwanza Vedastus Lufano alifika Uwanjani hapo kuishuhudia Pamba ikicheza na JKT Oljoro.