TAMASHA kubwa la NYANZA Featival linatarajia kuanza
kusaka vipaji mtaa kwa mtaa lengo likiwa ni kuhakikisha wanawafikia wasanii wote
chipukizi katika Nyanja zote za Music, Scrash dj, Dancer , Mitindo, Uigizaji na
uchekeshaji.
Akizungumza na Mwanza music House mwenyekiti wa
kamati ya maandalizi Fabian Fanuel wa alisema lengo ni kuhakikisha wanaibua
vipaji vyote na kuviendeleza.
“Ni muda sasa wasanii ambao ni underground wamekosa
nafasi ya kupanda jukwaa moja na wasanii
wenye majina makubwa ,licha ya jiji hili
kuwa na wasanii wengi na waliosheheni vipaji mbalimbali katika Nyanja zote”,
alisema Fanuel.
Fanuel alisema kuwa wanatarajia kuanzia mitaa ya Dampo,
Igoma, Mkuyuni , Nyegezi Buhongwa, Mabatini, Kisesa, Sahara, Buzuruga , National, Furahisa, Pasiansi Ilemela,
Igombe, Kiseke na Kiloleli.
“Sisi kama waandaaji tumejipanga vya kutosha
kuhakikisha wasanii wa Mwanza wanatanggaza vipaji vyao ni kazi itakuwa imebaki
kwao tu kuhakikisha waitendea haki fursa hii ambayo ni adimu kuipata tena”,
alisema Fanuel.
Alisema litakuwa tamasha la aina yake kutokana na
maandalizi na kuwataka wafadhili kuendeza kujitokza katika kuhakikisha
wanafanikisha tukio hilo muhimu linalotajia kufanyika katika sherehe za sikukuu
za Pasaka kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Nyanza
Festival 2017 linatorajariwa kufanyika kwa mara ya kwanza Jijini Mwanza na
baadaye kusambaa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, Tanzania na nje ya Tanzania ikiwashirikisha
wasanii wote kutoka jijini hapa.