Na Johnson
James , Mwanza
Simba
ilifanikiwa kuinasa saini ya mchezaji wa kimataifa wa Rwanda Haruna Niyonzima
ambaye ataitumikia Simba kwa mkataba wa miaka miwili nahodha wa timu hiyo Jonas
Mkude amesema kuwa yeye ndiye amechangia nyota huyo wa zamani wa APR ya Rwanda
kutua msimbazi.
akizungumza
na mwanzasportshouse katika mahojiano maalumu Jonas Mkude amesema kuwa yeye ndiye
alifanikisha mchongo wa mchezaji Haruna Niyonzima kutua Simba " kwanza
kabla ya niyonzima kuja Simba tulikuwa tukizungumza nikamshawishi aje
tutengeneze fomesheni kali katikati na akakubali hivyo kazi ikawa rahisi kwa
viongozi kumvuta hivyo tunategemea kufanya mazuri kwenye ligi ijayo"
alisema
Aidha Mkude
amesema kuwa Niyonzima ni mchezaji ambaye alikuwa anampenda na kukubali
uchezaji wake anapokuwa Uwanjani " Niyonzima nilikuwa nampenda sana
kutokana na jinsi anavyocheza lakini leo hii amekuja kwenye timu ninaychezea
mimi niwaahidi wapenzi wa Simba kuwa tumejipanga kufanya makubwa msimu ujao wa
ligi kuu Tanzania bara' aisema
Ikumbukwe
kuwa Mpaka sasa timu ya soka ya Simba imesajiri jumla ya wachezaji 10 ambapo
timu hiyo inajiandaa kufanya vema katika msimu ujao wa ligi kuu bara pamoja na
ushiriki wa michuano ya kimataifa ya kombe la Shirikisho barani Africa.