Na Johnson
James, Mwanza
Nahodha wa
timu ya Simba Jonas Mkude wikendi iiyopita alipewa tuzi ya keshima kutoka kwa
mashabiki wa Simba mkoani mwanza maarufu kama 'Simba task Force' kutokana na
mchango wake ndani ya klabu hiyo huku lengo kuu la kumpatia heshima hiyo ni
kukubali kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea timu hiyo.
Akizungumza
na Championi mara baada ya kumpatia tuzo hiyo mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo
hiyo Hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi wa
mkoa wa Mwanza Wilbert Martine Chuma
amesema kuwa lengo la tuzo hiyo ni kumpongeza na kutambua mchango wake
ndani ya Simba " mashabiki wa timu ya Simba Mwanza wameamua kumpa tuzo ya
heshima Mkude kutokana na kusaini mkataba mpya lakini pia mchang wake kwa timu hivyo
ninampongeza sana" alisema
kwa upande
wake Jonas Mkude ambaye hivi majuzi alisaini mkataba wakuitumikia Simba kwa
muda wa miaka miwili alisema kuwa anashukuru kwa heshima aliyopata " Mimi
nawashukuru mashabiki wa Simba Mwanza kwa kutambua mchango wangu katika timu
hivyo naahidi kujituma zaidi kuelekea msimu ujao ili Simba iwe tishio na wao
wafurahi zaidi" alisema
Mkude
ameongeza kuwa kimsingi atahakikisha kuwa anaendelea kujituma kwenye kazi yake
hivyo Mimi nitaendelea kujituma sana
kwani ndani ya Simba kunawachezaji wengi sana lakini kwa heshima niliyopewa
nitahakikisha kuw anajituma zaidi ili timu yangu ipate mafanikio.