Na Mwandishi wetu , Dar es salaam
Uchaguzi wa shirikisho la soka hapa nchini utafanyika agost 12 mwaka huu mkoani Dodoma, wakati uchaguzi huo ukitarajia kufanyika tayari mafahari wawili ambao ni aliyekuwa mwenyekiti wa Yanga Iman Madega na Rais wa sasa wa TFF na mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kagera Jamal Malinzi wamejitokeza kuchukua fomu ya kuwania urais wa Shirikisho hilo baada ya muda wake wa miaka minne kumalizika.
Lakini niwakumbushe wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa TFF kuwa wasichukue fomu kwa mazoea, kwani siku za hapo nyuma baadhi ya watu wamekuwa wakitumika kugombea nafasi na kumbe wanakuwa na malengo yao tofauti, watanzania kwa sasa wanahitaji maendeleo katika soka lao na hatutegemei watu kuchukua fomu kwa maigizo, watanzania wote tumekuwa mashahidi kwamba Rais wa sasa wa Soka hapa nchini Jamal Malinzi yapo baadhi ya mambo ameyafanya vizuri na mengine ametuangusha kama watanzania na kwa hapa tulipofika tunahitaji kiongozi ambaye ataitoa Tanzania hapa tulipo na kutupeleka sehemu tunayoihitaji,
Wakati nikiwa na miaka mitatu nikiwa nimeanza kazi ya Uandishi wa Habari za michezo kwenye gazeti la michezo la Championi nilikuwa nikifanya kazi na Silyvetre Marsh ambaye kwa sasa ni Marehemu wakti akikiendeleza kituo chake cha Marsh Athletics ghafla hali yake ilibadirika na akiwa katika hospitai ya muhimbili jijini Dar aifariki kwa ugonjwa wa kansa ya koo hiyo ilikuwa mwaka 2015 TFF walinishangaza pale ambapo walionyesha bifu zao na marehemu kwa kushindwa hata kumkodia ndege kwa heshima badala yake wakamuweka kwenye gari aina ya kosta eti kisa zilikuwa hazipandi na bwana mkubwa Malinzi hivyo hata laana hii ya Marsh itaendelea kumtafuta malinzi kwakua alionyesha kuwa na moyo wa kutokusamehe.
Na ukiachana na hilo sisi Watanzania tunahitaji maendeleo katika soka kwa kiongozi yoyote atakayefanikiwa kushinda uchaguzi huo kwani tumekuwa tukikosa timu bora ya taifa, tanzania imekuwa ikishuka kwenye viwango vya fifa kila kukicha lakini pia tumeshindwa kuitengeneza ligi yetu kuwa yenye ushindani lakini pia hata hawa viongozi wa TFF waliopo wamekuwa wakiingia mikataba ya udhamini kwa maslahi yao binafsi hivyo tunahitaji maendeleo zaidi kuliko porojo katika soka letu.