Na Johnson
James, Mwanza
Timu ya
waandishi wa habari jijni hapa maarufu kama Wanahabari fc imeichapa bila huruma
timu ya Veteran fc kwa jumla ya bao 2-1 katika mchezo wa mashindano ya
ramadahan cup uliopigwa Uwanja wa Mirongo jijini hapa.
Katika
mchezo huo uliokuwa na ushindani wa aina yake ulishuhudia mabao ya washindi
yakifungwa na Moses William aliyefunga bao la kwanza dakika ya 17 ya mchezo huo
kwa faulo kali baada ya mpira wa adhabu huku bao la pili likifungwa na Mark
Jerome huku lile la kufutia machozi kwa Veteran likifungwa na Julius Robert
dakika ya 80 ya mchezo huo.
Akizungumza
na Mtandao huu Nahodha wa timu ya wanahabari fc Moses William alisema kuwa timu
yake iko katika mazingira mazuri ya kutwaa kombe la ramadhan cup " mimi
timu yangu iko katika hali nzuri na matumaini yetu ni kulitwaa kombe la
ramadhan Cup kwani tunaowachezaji wazuri zaidi ambao tunaamini watatusaidia
kufanikisha ndoto zetu za kuwa mabingwa wa michuano hiii" alisema
aidha
William amewaomba wadau na wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja
wa shule ya msingi Mirongo kwaajili ya kushuhudia michezo ya ramadhan cup
" Sisi kama waandishi wa habarii tunaouwezo wa kufanya mambo mengine nje
ya taaluma yetu hivyo tunaomba ushirikiano
kutoka kwa mashabiki wetu wafike kutuunga mkono" alisema
leo majira ya saa 9 alasiri timu hiyo inatarajia kuingia uwanjani kukipiga na Lumumba fc .