Mechi
namba 4 Kundi C (Dodoma FC v Pamba). Meneja wa timu ya Pamba FC, Salmin
Kamau amepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa mwezi mmoja kwa kosa
la kutoa lugha chafu kwa mwamuzi. Adhabu dhidi yake imezingatia Kanuni
ya 41(2) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Viongozi.
Lakini pia Klabu ya Pamba imekuwaje Meneja wake Salmini Kamau afungiwe wakati waamuzi waliochezesha hovyo katika mchezo huo hawajachukuliwa hatua "haiwezekani Meneja wetu afungiwe wakati mwamuzi aliyecheza mchezo wa Dodoma fc na Pamba sc Clement Ntambi ambaye kimsingi alichezesha kwa viashiria vya maelekezo asichukuliwe hatua hivyo klabu ya Pamba itajua nini cha kufana kuhusu hilo" alisema kiongozi wa Pamba baada ya kupata taariffa kutoka TFF.