Timu ya soka ya Igoma Heroes ya jijini Mwanza jana ilifanikiwa kuichapa timu ya Iseni fc kwa jumla ya bao 3-2 katika mchezo wa ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Mwanza mchezo uliopigwa kwenye Uwanja mkongwe wa Nyamagana.
ligi hiyo kwa sasa inaendelea hatua ya 9 bora ambapo timu zinacheza majira ya saa8 mchana na saa 10 jioni na katika mchezo wa awali Black Mamba iliichapa Vijana fc bao 4-1 katika mchezo wa ligi hiyo.