Mshambuliaji muhimu wa timu ya soka ya Simba Ibrahim Ajibu ni kati ya walio tayari kwa ajili ya mechi ya watani wao Yanga, leo.
Simba inaivaa Yanga katika mechi nusu fainali ya ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar ambapo katika mchezo wa kufuzu kuingia nusu fainali Simba iiliichapa Jang;ombe boys kwa jumla ya bao 2-0 huku Yanga wao wakipokea kichapo cha bao 4-0 kutoka kwa Azam fc.
Ajibu ambaye amerejea nchini wiki iliyopita baada ya kufanya majaribio katik timu ya Haras El Hodood ya nchini Misri , ameanza mazoezi na wenzake na yuko tayari kwa ajili ya mechi ya leo “Ajibu naye yuko fiti, hapa ni chaguo la mwalimu Omog kama atamhitaji,” kilieleza chanzo.
Hata hivyo, kinachoonekana ni chaguo kubwa alilonalo Kocha Joseph Omog kwa kuwa pamoja na Ajibu, wako akina Mohamed Ibrahim, Pastory Athanas, Juma Luizio, Shiza Kichuya na wnegine wengi.