Izzo Bizness amefunguka kuhusu kuchelewa kwa kazi zake ambazo amefanya na rapper Nick wa Pili ambapo aliwahi kuahidi kuwa zitatoka muda si mrefu.
Akiongea na mtangazaji wa Maisha FM ya Dodoma, Silver Touch, rapper huyo amesema kuwa tayari ameshafanya nyimbo mbili na Nick na kwa sasa anaangalia muda muafaka wa kuziachia.
“Hapana Nick wa Pili tuna project nyingi ambazo tumeshazifanya, zipo kama mbili hivi. Ni mipango ya muda pia ngoma gani itoke,” amesema Izzo.
Rapper huyo wa kundi la Amazing ameongeza kuwa hivi karibuni amepanga kuja na kazi zake binafsi akiwa nje ya kundi hilo ambalo yupo na mrembo Abela Music.
source: Bongo 5
source: Bongo 5