MEXIME: TIMU
AMBAZO ZINAJILINDA KUSHIKA DARAJA HUWA NGUMU
siku moja
baada ya timu ya Kagera Sugar kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Toto
african katika mchezo wa ligi kuu bara uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba Kocha
mkuu wa Kagera Sugar Mecky Mexime amesema kuwa ukicheza na timu ambazo
zinaelekea kushuka daraja mchezo huwa mgumu kuliko kucheza na Simba au Yanga.
Mexime
alitoa kauli hiyo baada ya wachezaji wake kushindwa kupata matokoe na kuambulia
sare katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba ambapo katika mchezo huo
ulishuhudiwa Toto African wakicheza kwa
kujituma na kupelekea Kagera Sugar kushindwa kupata ushindi kwa Toto african.
akizungumza
na mtandao huu Kocha mkuu wa Kagera Sugar Mecky Mexime
amesema kuwa hakutegemea kupata upinzani mkubwa aliopata kutoka kwa Timu ya
Toto african " mimi nikiandaa kikosi changu kupata ushindi lakini Toto
walikaza na kupelekea kutoa sare ya mchezo wetu na ambacho nimegundua ukicheza
na timu ambazo ziko kwenye hatari ya kushuka daraja huwa zinabana sana lakini
tuliajiandaa kushinda" alisema
kwa upande
wake Kocha mkuu wa Toto african tim jost aisema kuwa kutokana na kuwa wako
katika hali mbaya katika msimamo wa ligi
wamejipanga kushinda michezo yao yote iliyosalia katika ligi kuu bara.