Na Janeth Joseph
Baada ya
wachezajii wa timu ya Stand United ya mjini Shinyanga kuwa katika mapumziko ya
wiki mbili sasa timu hiyo imeingia rasmi kambini kujiwinda na mzunguko wa lala
salama katika ligi kuu bara ambapo timu hiyo inatarajia kumenyana na African
Lyon april 2 mwaka huu uwanja wa Uhuru katika
mchezo wa ligi kuu bara.
Akizungumza
na Mwanza Music House Kocha msaidizi wa Stand United ya mjini Shinyanga Athuman Bilali
amethibitisha kuwa timu hiyo tayari iko kambini kuajiandaa na michezo ya ligi
kuu bara " kwa sasa tumeshaingia kambini kujiwinda na michezo iliyosalia katika ligi kuu hivyo
tumeingia mapema na dhumuni letu kuu ni kuhakikisha kuwa tunashinda michezo
yetu yote iliyosalia ili tuweze kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa
ligi" alisema
Aidha Bilali
amesema kuwa timu hiyo bado inakazi kubwa ya kufanya kwani mpaka sasa wana
pointi 28 ambapo kama wakishindwa kupata matokeo katika michezo yote iliyosalia
wanaweza kushuka daraja " mpaka sasa tuna pointi 28 baada ya michezo 24
hivyo bado tunakazi kubwa ya kuhakikisha kuwa tunashinda michezo yote
ili tuweze kusalia katika ligi" alisema