Simba kupitia kwa Makamu Mwenyekiti Geofrey Nyange Kaburu wanasema wanauhakika Kuwa Fakhi alicheza mchezo huo akiwa tayari ana kadi Tatu za njano jambo ambalo wanafahamu ya kuwa ni kinyume na kanuni za uendeshaji wa Ligi hivyo kuitaka kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi Kuliamua kwa Haki jambo hilo.
-Tunahitaji Alama Tatu, Ushahidi tunao ya kuwa Fakhi alipewa kadi Njano katika Michezo dhidi ya Mbeya City Disemba 17 Mwaka jana, pia Mchezo namba 165 dhidi ya African Lyon fc Januari 18 mwaka huu, na dhidi ya Majimaji Machi 4, mwaka huu hiyo kwa mujibu wa kanuni hakustahili kucheza mchezo dhidi yetu lakini Kagera Sugar walimpanga na kucheza’ Alisema Kaburu.
Wakati Kamati ya Uendashaji na Usimamizi ya Ligi Tanzania Kamati ya Saa 72 ikikaa Ijumaa April 7 kupitia Rufaa na malalamiko mbalimbali, Kagera Sugar kupitia kwa Kocha Mkuu Mecky Mexime wamesema Suala la Fakhi si la kweli kwani alikuwa Huru kucheza mchezo huo kwasababu alikuwa na kadi mbili za njano na tatu kama Simba wanavyosema..
-Sisi tupo makini sana na Masuala ya Kadi ya wachezaji, kila mchezaji anapooneshwa kadi tunaandika, Fakhi hakuwa na Kadi Tatu bali ana kadi Mbili, Simba kama wamshindwa mpira Uwanjani wasikimbilie kutafuta Ushindi wa mezani kimizengwe’ Mexime Alisema