Katika hali isiyokuwa ya kawaida tikezi za Elfu tano ambazo ndizo tiketi nafuu zaidi kuelekea mchezo wa Toto african dhidi ya Simba zimemalizika wakati zilipokuwa zikiuzwa kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini hapa muda huu .
Picha kama zinavyoonyesha watu bado ni wengi lakini wauzaji wanadai tikezi za majukwaani zimekwisha na zimebaki zile za VIP za shilingi 10000 ambazo wengi wanashindwa kuzimudu.
wakizungumza na Mtandao huu mashabiki wa soka ambao wamejitokeza kununua tiketi Uwanjani hapo wamesema kuwa wauzaji wanafanya makusudi kwani wanataka kuuza tiketi za bei kubwa ili wapate mapato mengi.