Baada ya
timu ya soka ya Simba kutwaa Ubingwa wa michuano ya kombe la FA kwa kuifunga
Mbao fc ya jijini hapa kwa bao 2-1 katika mchezo uliopigwa ndani ya dakika 120
kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Kocha mkuu wa timu ya Mbao Ettiene Ndayiragije raia wa Burundi amesema kuwa timu yake haikuwa na habati
katika mchezo ndiyo maana walishindwa kuibuka na ushindi.
Akizungumza
na Championi kwa njia ya simu kutoka mkoani Dodoma Ettiene Ndayiragije amesema
kuwa timu yake ilicheza kwa kiwango kizuri lakini bahati haikuwa upande wao
" sisi tumecheza vizuri na tulifanya kila kitu lakini naweza kusema bahati
haikuwa kwetu kama mlivyoona tumecheza dakika 120 hii yote ni kujituma kwa
wachezaji wangu ambao walilihitaji hili kombe lakini Bahati haikuwa yetu"
alisema
aidha
Ettiene ameongeza kuwa Simba ni timu kubwa lakini katika mchezo ule wa fainali
walishindwa kuoyesha ukongwe wao " Mimi niwapongeze wachezaji wangu kwa
kucheza vizuri na timu ambayo ni kongwe katika soka la Tanzania hivyo
tutajipanga kunako michuano ijayo ili tuweze kutimiza ndoto za kuiwakilisha
nchi katika michuano ya kimataifa hivyo nawapongeza hata Simba kwa kutwa kombe
hili la Azam" alisema
Ndayiragije
amewapongeza mashabiki wa Mbao fc ambao walijitokeza kwa wingi katika Uwanja wa
jamhuri mjini Dodoma kuisapoti timu yao licha ya kushindwa kutwaa ubingwa wa
kombe la FA " niwapongeze mashabiki wetu ambao walisafiri kutoka Mwanza
kwenda Dodoma kwaajili ya kuisapoti timu yao licha ya kutotwaa ubingwa mchango
wao ulionekana tangu mwanzo wa mchezo mpaka mwisho"
Chanzo: Championi jumatatu.