Na Johnson
James, Mwanza
Timu ya soka
ya Alliance Sports Cademy inayojiandaa kushiriki ligi draja la kwanza msimu
ujao imemtangaza aliyekuwa Kocha mkuu wa
timu ya Tanzania Prison, Kagera Sugar na KMC ya Dar es salaam Mbwana Makata kuwa kocha wake mkuu ambapo
ataiongoza timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmkoja huku lengo la kutangazwa kwake
ikiwa ni kuhakikisha kuwa timu hiyo inapada daraja licjeza ligi kuu bara msimu
ujao.
Akizungumza
na Championi Mwenyekiti wa kamati ya
Mashindano ya Alliance Yusuph Budodi amesema kuwa wameamua kumtangaza kocha
huyo kutokana na kuwa na vigezo vya kuipandisha daraja timu hiyo "
kimsingi sisi kama Alliance tumeamua kumtangaza Kocha Mbwana Makata kutokana na
uzoefu wake na amesaini kataba wa mwaka mmoja kuifundisha timu yetu na moja ya
mambo mbayo tumekubaliana ni kuipandisha daraja timu yetu baada ya kushindwa
kupanda msimu uliomalizika" alisema
kwa upande
wake Kocha Mbwana Makata ambaye amewahi kuzifundisha timu za Toto african,
Kagera Sugar pamoja na Tanzania Prison kwa mafanikio makubwa amesema kuwa
amejipanga kuhakikisha kuwa anatimiza ndoto za Alliance kucheza ligi kuu "
Nashukuru sana Alliance kwa kunichagua mimi kuifundisha timu yao na ninawaahidi
kuwa nitahakikisha kuwa Alliance inapanda daraja msimu ujao kwani msimu
uliopita walikosa pointi tatu tu kupanda" alisema
aidha Makata
amewahakikishia viongozi wa timu ya Aliance kuwa timu hiyo lazima ifikie
malengo yake " Nimezungumza na Uongozi wa Alliance na tumekubaliana sana jinsi ya kuiendesha timu hiyo na mimi
wamekubali maoni yangu na imani tutafanya vizuri zaidi kuelekea msimu ujao wa
ligi daraja la kwanza.
Ikumbukwe
kuwa timu ya Alliance sports academy msimu uliomalizika ilishindwa kupanda
daraja kundi C baada ya kuzidiwa pointi 3 na Singida United ambao walipanda
daraja kwa pointi 31 huku Alliance wakishindwa kupanda daraja baada ya kuw ana
jumla ya pointi 29 .
Chanzo: Championi.