Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
Klabu ya Simba Leo Jumanne imemtambulisha Rasmi mshambuliaji John Bocco Adebayor katika Timu hiyo kwa Mkataba wa miaka miwili wenye Thamani ya shilingi Milioni 40.Bocco anatua Simba SC baada ya Misimu Kumi akiwa na Azam FC ambayo alijiunga nayo mwaka 2007 akitokea Cosmopolitan ya Dar es Salaam na akaisaidia Azam FC, kupanda Ligi Kuu mwaka 2008 akiibuka mfungaji bora wa Daraja la Kwanza. Baada ya hapo, Bocco akawa mshambuliaji tegemeo wa Azam FC akiiongoza kutwaa mataji kadhaa, ikiwemo Ligi Kuu mwaka 2014 na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, au Kombe la Kagame mwaka 2015. Na sasa anakuja Simba akitarajiwa kuleta upinzani mkubwa wa nafasi hiyo mbele ya wachezaji Laudit Mavugo na Juma Luizio.
Bocco anakuwa mchezaji wa Tatu Kusajiliwa na Simba SC akitokea Klabu ya Azam FC ambapo awali Simba waliwatambulisha mlinda mlango Aishi Manula na beki Kisiki Shomari Kapombe.