Na Johnson James, Mwanza
Ettiene Ndayiragije ni Kocha mkuu wa Mbao fc raia wa Burundi ambaye ameishangaza Tanzania baada ya kuiongoza timu ya Mbao fc ambayo imepanda daraja kucheza ligi kuu kwa mara ya kwanza na kutoshuka daraja na kisha kutinga hatua ya kucheza Fainali ya kombe la Azam federation kwa mara ya kwanza huku timu hiyo ikikwepa kushuka daraja kwa kuichapa timu ya Yanga kwa bao 1-0 katika mchezo wa kuhitimisha ligi, Championi ijumaa limezungumza na Kocha huyo ambaye amefunguka mengi kuhusu soka la Tanzania na mstakabali wake ndani ya Mbao fc
Ulitumia mbinu gani kuijenga mbao na kuwa moja ya timu ambazo zimefanya vizuri katika ligi?
Katika kujenga timu kila Kocha anambinu zake au falsafa ambazo anaamini zinaweza kumsaidia kufanya vema katika timu yake na kwa upande wangu kuna mambo ambayo niliyaamini kuwa yatanisaidia na nilipowafanyia wachezaji wangu zikasaidia hivyo siwezi kusema moja kwa moja nilifanyeje lakini uhakika ni kwamba ili timu ifanye vizuri lazima kocha afundishe mambo yake na wachezaji wakielewa timu lazima iwe tishio"
kwanini timu yako inacheza kwa kukamia simba na Yanga?
" Nikweli kabisa timu yangu imekuwa ikizisumbua timu za Simba na Yanga na mimi ninapocheza na mpinzani wangu huwa naangalia nini anafanya namimi najiandaa kivingine hivyo kitu kilichopelekea timu yangu kufanya vizuri katika michezo ya hivi vilabu viwili ni jinsi ambavyo niliwaandaa wachezaji wangu kisaikolojia lakini pia liikuwa nawafuatilia hivyo hata mimi nilikuwa na mbinu zangu ambazo kila nilipozitumia hizi timu zilipata tabu sana nadhani kila mtu alikuwa akishuhudia kitu wachezaji wangu walikuwa wakifanya hivyo ifahamike kuwa sisi Mbao hatuzikamii Simba na Yanga bali tunafanya maandalizi ambayo yanatuwezesha kufanya vizuri"
Umefundisha Mbao inayoshiriki ligi ya Tanzania , umeona tofauti gani kati ta ligi ya Tanzania na Burundi?
Kwanza ukishasema Tanzania na Burundi tayari hiyo ni tofauti lakini niseme kwamba ili uweze kushiriki ligi ya Tanzania lazima timu yako iwe na uwezo wa kiuchumi kwani nimeona timu zinasafiri umbali mrefu sana tofauti na Burundi kwani timu kama inafedha za kutosha inaweza kufanya vizuri zaidi kwenye ligi ya Tanzania kwani nimeona hapa Mbao tumesafiri sana tunatumia pesa nyingi kwenye hoteli hivyo ili ufanye vizuri kwelie ligi ya Tanzania lazima uwe na fedha za kutosha"
umeonaje ushindani katika ligi ya Tanzania??
" Kiukweli ushindani katika ligi ya Tanzania ni mkuba sana kwani nimeshuhudia timu zikicheza kwa nguvu sana na kilichonishangaza zaidi ni pale ligi inafika mwisho hajulikani nani atashuka daraja hivyo kwa jinsi nilivyoona ushndani ni mkubwa sana na Mashabiki wanapenda sana timu zao kwani wengi tumeona jinsi ambavyo mashabiki wa Simba na Yanga walivyokuwa wanakuja kuziona timu zao walipokuwa wamekuja kucheza na Mbao na Toto hivyo ushindani ni mkubwa sana kwa timu zilizo shiriki"
Vipi Mpango wako wa kusalia Mbao fc
" Kwanza kwa sasa siwezi kuzungumzia kuhusu kubaki Mbao kwani Mkataba umekwisha kwani ulikuwa wa mwaka mmoja na nasubiri ofa ya viongozi wangu wa Mbao ili tuone jinsi gani ya kufanya lakini kitu kilichokuwa kikiniumiza kichwa nilikuwa nagojea shukrani na nimefurahi sana baada ya kuona Uongozi wa Mbao fc umekubali mchango wangu hivyo baada ya mkataba wangu kuisha nawapa nafasi ya kwanza wao kwanza na nina imani kuwa nitasalia Mbao fc kwa msimu ujao"
Timu gani zimeonyesha nia ya kukuhitaji?
Tena naomba niliweke sawa hili kwanza ukiwa wewe ni profesheno unapaswa kuheshimu mkataba na kazi yako kwani unakuwa bado ni mfanyakazi hivyo kwa kipindi kilichopita nisingeweza kuzungumza na timu yoyote ili niifanyie kazi kwani naheshimu sana kazi yangu na ikumbukwe mpaka ligi inamalizika nilikuwa na mechi kubwa ambazo zinapresha sana na ilifikia kipindi nikawa sipokei hata simu yote haya ni kuhakikisha kuwa Mbao fc inakuwa katika mikono salama ya kutoshuka daraja hivyo hakuna timu niiyozungumza nayo wala nisingeweza kuzungumza nao wakati bado nina mkataba na Mbao fc".
Kocha mkuu wa Mbao fc Ettiene Ndayiragije akiwa na Kocha wake msaidizi Soud Slim Kulia.
Mipango yako ndani ya Mbao fc
" Mipango yangu ndani ya Mbao fc nitaiweka sawa endapo nitakubaliana na viongozi wangu kuhusu mkataba wangu na hapo ndipo nitazungumzia mipango yangu lakini kwa sasa mipango iliyokuwepo ilikuwa ni kuibakisha Mbao ligi kuu imebaki na sasa lazima tuje na mipango mingine na nitazungumzia hilo nikishasaini mkataba upya na uongozi wa Mbao fc"
Mchezaji gani aliyekuvutia katika ligi iliyomalizika?
" Kiukweli wapo wachezaji wengi ambao walionekana kunivutia katika ligi ya Tanzania lakini kiboko yao ni mchezaji wa timu yangu Yusuph Ndikumana kwangu ndiye alistahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora kwani alipofika Mbao kiwango chake kilikuwa kidogo lakini mpaka tunamaliza ligi nimemuona Ndikumana Mwingine kabisa hivyo najivunia sana kuwa na Ndikumana kwenye timu yangu lakini pia Ndikumana ndiye nahodha wa timu yangu hivyo nilifurahia uongozi wake awapo uwanjani alihakikisha kuwa wachezaji wanakuwa na nidhamu hivyo ni mchezaji ambaye amenivutia kwakweli"
Umepewa jukumu la kuzungumza na wachezaji wako wasihame Mbao hili utalifanya kwa asilimia ngapi?
" Nimepewa jukumu kubwa sana na nitajaribu kukaa nao niwashauri kipi wakifanye kwa manufaa yao ya badae kwani endapo mchezaji yoyote wa Mbao akiondoka kwa tamaa tu haitamsaidia hivyo nitahakikisha kuwa wachezaji wote nazungumza nao vizuri nitawaelekeza lakini mwisho wa siku ambaye hataelewa yatakuw amaamuzi yake kuondoka hivyo nitaifanya hiyo kazi"
Umebaini mapungufu gani kwa ligi ya Tanzania
" Tatizo kubwa ambalo nimelibaini katika soka la Tanzania ni timu ambalo ni timu ndogo kukosa udhamini kwa hali hiyo mchezo wa soka hauwezi kuendelea hata kidogo kwani nimewaona Sports Pesa wanatoa udhamini kwa timu kubwa tu za Simba na Yanga na Singida United kidogo kitu ambacho nakiona sio sawa hivyo naona kwamba ili ligi kuu iwe na ushindani wa aina yake lazima vilabu vyote bila kujali udogo wao vipate udhamini ambao utawawezesha kushindana na endapo wakijitokeza wadhamini kuzidhamini timu ndogo hakika ligi ya Tanzania itakuwa ligi bora africa lakini bila udhamini Tanzania wataendelea kupiga marktime"
Vipi kuhusu falsafa yako ya kuamini vijana
"Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zina vijana ambao wanaweza kucheza soka lakini wanakosa wa kuwasaidia mimi falsafa yangu nitaendelea kuwaamini vijana na naliomba shirikisho la soka hapa nchini kuwe na waalimu maalumu wa kuchunguza vipaji vya vijana ambao mwisho wa siku watakuja kulisaidia taifa kwani kwenye timu yangu wachezaji ambao wamefanya vizuri zaidi ni wale ambao niliwatoa kwenye timu ya Mbao fc ya vijana hivyo TFF iweke mikakati ya kukuza vipaji vya hawa vijana"
Timu iliyokusumbua katika ligi
" Kiukweli zipo timu nyingi ambazo zilinisumbua katika ligi lakini timu iliyonisumbua ni timu ya Mbao fc ambayo naifundisha mwenyewe kwani kuna wakati wachezaji walipokuwa wanapata mahitaji yao walikuwa wakicheza vizuri lakini wakikosa mahitaji yao muhimu walikuwa wanagoma kucheza hali hiyo ilikuwa inanikosesha sana Amani hivyo yapo Mambo mengi sana ambayo yananipelekea niseme Mbao ndiyo timu ilinisumbua sana zaidi ya timu yoyote "