TETESI KUTOKA BARANI ULAYA TAR. 12/06/2017
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ana uhakika mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, atajiunga na klabu hiyo - kwa ofa inayotarajiwa kutolewa siku ya leo Jumatatu. (Chanzo Marca)
Morata ameonyesha kwenye mtandao wa kijamii kuwa anaweza kujiunga na United, baada ya ‘Kulike’ posti ya Instagram iliyokuwa ikionekana kuthibitisha uhamisho wake. (Chanzo Metro)
United huenda wakamuongezea Zlatan Ibrahimovic, 35, mkataba wa muda mfupi, licha ya kumruhusu, ikiwa mshambuliaji huyo wa Sweden atafanikiwa kupata nafuu kutokana na upasuaji wa goti. (Chanzo Manchester Evening News)
Paris St-Germain wamepiga hatua kubwa kuelekea jitihada zao za kumsajili mshambuliaji wa Monaco mwenye umri wa miaka 18 kutoka nchini Ufaransa Kylian Mbappe, ambaye anasakwa pia na Arsenal, Chelsea pamoja na Manchester United. (Chanzo L'Equipe - kwa Kifaransa)
Chelsea wanataka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Real Madrid kutoka nchini Colombia, James Rodriguez, 25. (Chanzo AS - kwa Kihispania)
Liverpool wako tayari kufanya jaribio la mwisho kumzuia kiungo Alex Oxlade-Chamberlain, 23, kusaini mkataba mpya wa paundi 100,000 kwa wiki na Arsenal. (Chanzo Daily Express)
Manchester United wako karibu kukubali usajili wa kiungo wa Monaco kutoka Brazil Fabinho, 23. (Chanzo Manchester Evening News)
Winga wa Algeria Riyad Mahrez, 26, amekili kuna uwezekano wa yeye kuendelea kusalia Leicester City kwa msimu mpya, licha ya kuweka wazi azma yake ya kuondoka klabuni hapo msimu huu wa majira ya joto. (Chanzo Leicester Mercury)
Mahrez anasema bado hajapokea ofa yoyote rasmi. (Chanzo Elheddaf Television kupitia Sky Sports)
Soka la mlinda mlango wa Manchester City Joe Hart na England huenda likawa hatarini, kwani hakuna klabu yoyote iliyotoa ofa kwa golikipa huyo mwenye umri wa miaka 30 baada ya kuitumikia kwa mkopo klabu ya Torino. (Chanzo Daily Mirror)
West Ham wako tayari kutoa ofa kwa Hart ya kuhamia Premier League. (Chanzo Sun)
Beki wa Ufaransa Laurent Koscielny, 31, amejiweka mbali na ripoti zinazomuhusisha na kuhamia Marseille, akisema ana furahia hapo Arsenal. (Chanzo Telefoot kupitia ESPN)
West Brom na Newcastle wote wanamtaka mshambuliaji wa Celtic kutoka nchini Scotland Leigh Griffiths, 26. (Chanzo Daily Mirror)
Mshambuliaji Emmanuel Adebayor amebaini kuwa uamuzi mbaya alioufanya katika soka lake ulikuwa ni ule wa kujiunga na Crystal Palace, ambapo alifunga bao moja tu katika mechi 15 mwaka jana. (Chanzo Daily Mirror)
Golikipa wa Italia Gianluigi Donnarumma, 18, atatia saini ya mkataba mpya na AC Milan. (Chanzo Corriere dello Sport - kwa Kiitalia)
Barcelona wanatarajiwa kutoa dau la paundi millioni 88 kwa Marco Verratti baada ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 kudai kwamba anataka kuondoka Paris St-Germain. (Chanzo Daily Mail)