Fifa kutuma wajumbe maalumu kuchunguza kinachoendelea juu ya viongozi wa Tff Jamali Malinzi,katibu mkuu Mwesigwa pamoja na mwanama Isende Mwanga wanaoshikiliwa na jeshi la polisi kwa makosa ya kugushi na utakatishaji wa fedha mashtaka ambayo walisomewa jana katika mahakama ya Kisutu.
Wakati ujumbe huo wa fifa ukitaraji kutua nchini wakati wowote kutoka sasa imeelezwa kuwa ujumbe huo wa Fifa utakuwa na kikao na viongozi wa Tff jumanne ijayo.
Kwa mengi zaidi usikose kusikiliza E.sports ya @efmtanzania leo usiku ambapo utamsikia makamo wa rais wa Tff Walles Karia akieleza kwa kina zaidi juu ya taarifa hiyo na ikiwemo suala la pingamizi lake alilowekewa.
Je,unajua kinachoendelea juu ya sakata la pingamizi lake,,?Tega sikio Shughuli imekuwa nzito.