Na Mwandishi wetu Munich, German
Timu za Manchester United na Chelsea zote za nchini England zimeingia katika vita ya kumuwania mshambuliaji wa timu ya Bayern Muchen Robert Lewandowski baada ya kuelezwa kuwa mchezaji huyo hana furaha katika kikosi cha Bayern Munich ya Ujeruman kutokana na wachezaji wenzake kushindwa kumpa ushirikiano ambao ungemuwezesha kutwaa kiatu cha ufungaji bora msimu uliomalizika ambapo mchezaji kutoka nchini Ghaboni Piere Aubameyang ndiye alitwaa tuzo hiyo kwa kufunga mabao 31 huku Lewandowsk akifunga mabao 30 pamoja na asist 5
Habari zaidi kutoka kwa wakala wa mchezaji huyo Maik Marthel amewalalamikia Uongozi wa timu hiyo na wachezaji wenzake kwa kushindwa kumpa ushirikiano wa kutosha mchezaji huyo ili aibuke kuwa mfungaji bora wa Bundesliga msimu uliomalizika Robert Lewandowski aliyesaini mkataba kusalia Bayern mpaka desemba 2021 anaweza kuondoka klabuni hapo endapo mabosi wa timu hiyo wakiridhia aondoke. Endapo mabosi wa Muchen wakiridhia Manchester United na Chelsea zinapewa nafasi kubwa ya kumtwaa mchezaji huyo.