Na Mwandish wetu England
Majogoo wa jiji Liverpool wapo karibu kumsajili mchezaji mwenye miguu yenye gundi ya''OKO''Mohamed Salah kutoka As Roma,katika usajili wa utakaogharimu kiasi cha pauni milioni 39 ambapo itakuwa ni rekodi kwa klabu hiyo kongwe nchini England.
Mchezaji huyo raia wa Misri mwenye umri wa miaka 25 aliyewahi kukipiga Chelsea amekuwa chaguo kuu la kocha Jurgen Klopp msimu huu.
Mazungumzo yanaendelea baina ya vilabu hivyo viwili,Salah mwenyewe ni mwenye furaha kurejea tena kucheza katika ligi Kuu ya England(Premier League)baada ya kuwa na wakati mgumu ndani ya kikosi cha Chelsea mwaka 2014.