Baada ya kusubiliwa kwa muda mrefu na wadau wengi wa mchezo wa soka hapa nchini hatimaye Ally Mayay Tembele mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga na timu ya Taifa amechukua fomu ya kugombea Urais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 12 Mjini Dodoma.
Nyota huyu wa zamani wa Yanga SC na Taifa Stars ameungana na mchezaji mwenzake wa zamani, Mtemi Ramadhan ambaye amejtosa kuchukua fomu ya kugombea umakamu wa Rais.
Mayay anatajwa kuwa, huenda akawa mpinzani mkuu kwa Rais anayetetea nafasi yake, Jamal Malinzi. kutokana na kuwa moja kati ya wadu wa kubwa wa mchezo wa soka hapa nchini, Tanzania kwa sasa inahitaji Viongozi ambao wanauelewa na kuujua mpira kiundani zaidi hivyo matarajio ya Wanzania waliowengi hapa nchini ni kuona Ally Mayay anashinda kiti cha Uraisi wa TFF.
Baadhi ya wadau wa soka hapa nchini wakiongozwa na Jamhuri julio wakimsindikiza kuchukua fomu Ally Mayay wakiwa na bango lililoandikwa Bring Back Our Ball wakimaanisha turudishie mpira wetu.
Baadhi ya wadau wa soka hapa nchini wakiongozwa na Jamhuri julio wakimsindikiza kuchukua fomu Ally Mayay wakiwa na bango lililoandikwa Bring Back Our Ball wakimaanisha turudishie mpira wetu.