Na Mwandishi wetu England
Baada ya Antonio Conte kuiongoza Chelsea kutwaa Ubingwa wa ligi kuu Nchini England Mchambuzi wa maswala ya michezo ulimwenguni Martin Samuel ambaye huandikia gazeti la mtandaoni la Daily Mail amemjia juu Meneja wa timu ya Chelsea muitaliano Antonio Conte na kusema kuwa kamwe meneja hawezi kuwa na nguvu kuliko bosi wake, Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Kocha huyo kumuandikia ujumbe mshambuliaji wa timu ya Chelsea muhispaniona Diego Costa kuwa hana mpango naye msimu ujao wa ligi kitendo ambacho kimetafsiriwa kuwa kinaweza kuwagawa wachezaji na kuifanya timu hiyo ishindwe kufanya vema katika ligi kuu nchini England msimu ujao ambapo timu hiyo inatarajia kushiriki michuano ya Uefa Champions League baada ya kuikosa ligi hiyo msimu uliopita.
Ikumbukwe kuwa Kocha wa sasa wa Manchester United Jose Mourinho alitwaa Ubingwa wa nchini England lakini kutokana na yeye kuwa na mgogoro na baadhi ya wachezaji alitimuliwa siku chache baada ya ligi kuanza, kadhalika Kocha Roberto Dimateo alitwaa Ubingwa wa Uefa Champions League lakini kutokana na kuwa na migogoro na baadhi ya wachezaji pia mwaka mmoja badae alitimuliwa bila kujali heshima aliyoipatia chelsea baada ya kutwaa kombe hilo, hivyo mchambuzi huyo wa maswala ya michezo amemtahadhalisha Antonio Conte kuwa akiendelea na mikwara yake Tajiri wa Chelsea Roman Abramovich atamtimua huku akiwa hana muda mrefu kwani ikumbukwe kuwa Tangu Tajiri Roman Abramovich ainunue Chelsea huu ni mwaka wa 14 na tayari ameshawatimua kazi makocha 12 mbali na wale makocha wa muda ambao ni Ray Wilkins pamoja na Steve Holland na ifahamike kuwa Chelsea kamwe haitapata mtu kama Kocha wa Arseno Arsene wenger au kocha wa Zaman wa Manchester Sir Alex Ferguson ambao wamezifundisha timu zao kwa muda mrefu hivyo Konte anatakiwa kubadirika kabla ya kutimuliwa na kuletwa kwa kocha mwingine atakayeendana na upepo wa Stamford Brigde.