Timu ya soka
ya Mbao fc yenye maskani yake wilayani Ilemela ambayo ilikuwa tishio katika
ligi kuu bara kwa timu za Simba na Yanga msimu wa uliomalizika inatarajia
kuanza maandalizi yake ya ligi kuu bara msimu ujao julai 3 mwaka huu ambapo
maandalizi kuelekea kambi hiyo tayari yamekamilika.
Mwenyekiti
wa timu ya Mbao fc Solly Njashi amesema kuwa kila kitu kiko tayari kuelekea
kambi hiyo " tayari Kocha wetu Ettiene Ndayiragije amewasili nchini baada ya kuwa kwenye
mapumziko nchini Burundi na kimsingi
tumejipanga kuhakikisha kuwa Mbao fc inaendelea kuwa tishio katika ligi kuu
bara " amesema
aidha Njashi
amesema kuwa licha ya kuondokewa na nyota wake kadhaa hilo halitawaumiza kichwa
bali watapata wachezaji wengine " sisi kama Viongozi tayari tumefanyia
kazi ripoti ya mwalimu ambapo yapo
baadhi ya mambo alipendekeza yafanyike na sisi tunatekeleza kama yalivyo ili
aweze kutekeleza mipango yake kwa uhuru zaidi
kama alivyopanga hivyo Mbao hatutaki mchezo katika ligi kuu bara msimu
ujao "alisema
aidha Njashi
amewaomba wachezaji wake ambao wako mbali wafike kambini mara moja kwaajili ya
kuanza maandalizi ya ligi msimu ujao " nawaomba wachezaji wangu wafike
kambini mapema ili tuanze maandalizi yetu kwan tumejipanga vizuri zaidi
hatutaki kunusurika kushuka daraja tena bali tunahitaji kuwa na pointi nyingi
ambazo zitatuwezesha kuwa sehemu salama zaidi kwenye ligi hivyo tumejipanga
kiukweli" alisema
Chanzo: Championi