Na Johnson
James, Mwanza
Wakati
wachezaji wa nchi za wenzetu wakinufaika na umaarufu wao ikiwemo kuwa mabalozi
wa vivuti mbalimbali katika nchi zao kwa hapa Tanzania imekuwa tofauti ambapo
wahifadhi wa mbuga zetu hususa watu wa TANAPA wameshindwa kuwatumia wachezaji
wazawa ambao ni maarufu kuutangaza utalii wao wa ndani ambapo kama wakifanya
hivyo wanaweza kupata faida kubwa.
Nahodha wa Simba Jonas Mkude wa kwanza kushoto akifuatilia maelezo kutoka kwa mwongozaji wa Kisiwa cha saa nane, picha zote na Johnson James,
Wikendi
iliyopita Nahodha wa timu ya Simba Jonas Mkude alikitembelea kisiwa cha saa
nane kilichopo jijini Mwanza na kujionea wanyamba mbalimbaliakiwepo Pundamilia, Ngedere, swala na wengine ambao wanapatikana
katika hifadhi hiyo, Mkude amefanya hivyo kwa matakwa yake binafsi lakini kama
TANAPA wangemtafuta ili awe balozi wao kimsingi wangepata faida kubwa sana
kwani angewahamasisha mashabiki wake na wao kuja Mbugani kufurahia wanyama,
lakini mimi niliyekuwa na Mkude mpaka anatoka hifadhini hapo hakuna hata
kiongozi yoyote aliyemfata hata kumsalimia ukizingatia ni maarufu sana kwa
mashabiki wa Simba.
hivyo mimi
nashauri wahusika wa kutangaza vivutio vya utalii hapa nchini wawatumie
wachezaji wa ndani kutangaza vivutio vyao kwani watapata faida kubwa sana mfano kwa sasa
Mkude anamaashabiki wake zaidi ya milioni 2 kama akiwa balozi wa vivutio vya
utalii nusu ya mashabiki wake watalazimika kutembelea pale staa wao
alipotembelea hivyo tukiwatumia wachezaji kutangaza vivutio tutaifanya Tanzania
kuwa kama sehemu fulani maaarufukuliko zote hapa Duniani kwani tunakivutio kama
Ngorongoro kreta lakini hatuitangaza wakati dunia nzima inapatikana Tanzania.
Nahodha wa Simba Jonas Mkude akifurahi na wanyama wanaopatikana kisiwa cha saa nane jijini Mwanza wikendi iliyopita baada ya kutembelea kisiwani hapo,