Na Johnson
James, Mwanza
Wakati timu
mbalimbali hapa nchini zikiendelea la usajiri wake kwaajiili ya kuimarisha
vikosi vyao kuelekea msimu ujao wa ligi Uongozi wa timu ya Pamba kupitia kwa Mratibu
wa timu hiyo Bob Butambala amesema kuwa watahakikisha kuwa wanaitengeneza Pamba
ambayo itapanda daraja kucheza ligi kuu bara msimu ujao kutokana na kushindwa
kupanda daraja muda mrefu.
Akizungumza
na Mwanza sports house mratibu wa timu ya Pamba fc Bob Butambala amesema kuwa kwanza ili
Pamba ifanye vema wanahitaji kuwa na viongozi bora ambao wataisaidia Pamba
kufanya vema kwenye ligi " kwa sasa tuko tunapanga safu yetu ya Uongozi
ambayo itatuwezesha kufanikisha malengo yetu kwani mwaka huu tumepania kuliko
miaka yote iliyopita kwani mipango yetu ni kuwarudisha wadau halisi wa Pamba ambao tunaamini wataisaidia tiu yetu kupanda daraja"
aidha
Butambala amesisitiza kuwa watahakikisha kuwa wanafanya usajiri wa
wachezaji wazuri na wenye uwezo ambao
wataisaidia timu hiyo kutimiza malengo
yake " kuelekea ligi daraja la kwanza msimu ujao tumejipanga kufanya
usajiri mzuri ambao kwa hakika utamaliza kiu ya wanamwanza kuiona tena Pamba
ikicheza ligi kuu msimu huu haututanii na tumejipanga sawasawa ili Pamba iwe
kama ile ya zamani" alisema
Ikumbukwe
kuwa mpaka sasa mkoa wa Mwanza una jumla ya timu tatu ambazo msimu ujao
zitashiriki ligi daraja la kwanza , timu hizo ni pamoja na Toto african
iliyoshuka daraja msimu uliopita, Alliance sports academy pamoja na timu ya
Pamba fc maarufu kama Tipi lindanda ambayo msimu uliomalizika ilishindwa kupanda daraja baada ya kutofanya
vema katika kundi lake la B.