MALINZI KUUKOSA URAIS TFF

Juni 29, 2017
Picha : Rais wa sasa wa TFF Jamal Malinzi kushoto akizungumza na Mwenyekiti wa soka la Vijana Ayoub Nyenzi kulia.

Na Mwandishi wetu, Dar es salaam.


Malinzi hataweza kukidhi vigezo vya Kuwania tena nafasi ya Urais wa TFF kwa mara nyingine  kwa kuwa kesi iliyomfikisha mahakamani leo itasikilizwa tena Jumatatu Julai 3 na Malinzi atakaa rumande hadi siku hiyo ambapo siku ya mwisho ya usaili kwa viongozi wanaogombea ni julai 1 mwaka huu .

Usaili wa viongozi wanaogombea uongozi TFF unafanyika kuanzia leo hadi keshokutwa wakati huo Malinzi atakuwa mahabusu huku kukiwa na baadhi ya wagombea ambao wamewekewa mapingamizi, 
Malinzi amefikishwa leo mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam akiwa na katibu wake, Mwesigwa Celestine.

Baadhi ya mashitaka hayo ni kughushi waraka wa kamati ya utendaji ulioonyesha kuwa imeridhia kubadilishwa kwa Signatories (watu wanaosaini nyaraka za benki kutoa fedha). Shitaka hilo linawahusu Malinzi na Mwesigwa.

Malinzi amedaiwa kugushi risiti za kwamba anaidai TFF na ziko risiti 20 ambazo anatuhumiwa kuzifoji.


Shitaka jingine ni utakatishaji na hii wote watatu, Malinzi, Mwesigwa na Nsian wanatuhumiwa kutakatisha kiasi cha dola 375418.

last post see below

Next Article
« Prev Post
Previous Article
Next Post »
PEOPLE WHO COMMENT BELOW POST DROP YOUR OPINION
  • use this code to select difert type of word with bold use <strong></strong> or <b></b>.
  • for the italic use <em></em> or <i></i>.
  • To write letters underline use <u></u>.
  • To write letters strikethrought use <strike></strike>.
  • To write code HTML use <code></code> atau <pre></pre> atau <pre><code></code></pre>, And please put The code in the parser box below.

Disqus
OkUser Add your comment

Hakuna maoni