AVEVA , KABURU RUMANDE MPAKA JULAI 13 MWAKA HUU

Juni 29, 2017
Rais wa Simba Evans Aveva (kulia) na Godfrey Nyange Kaburu wamepelekwa Rumande baada ya kukabiliwa na mashitaka matano ikiwemo ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana.
Washitakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutakatisha fedha ambayo ni dola za Marekani 300,000 walizozipata kwa kughushi nyaraka kuonesha kwamba Club ya Simba imelipa deni la fedha hiyo kwa Aveva.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisema mashitaka hayana dhamana hivyo aliahirisha hadi Julai 13 mwaka huu kujua hatua ya upelelezi umefikia wapi.
MAKOSA 5 YALIYOTAJWA KWENYE KESI
Makosa 5 yanayowakabili Rais wa Simba Aveva na makamu wake Kaburu
1. Kughushi,..
Aveva alighushi nyaraka ili kujilipa deni ambalo inadaiwa aliikopesha Simba USD 300,000.
2. Nyaraka za uongo
Walitumia nyaraka za uongo ili kulipa deni kutoka benki ya CRDB.
3. Kutakatisha fedha 
Tarehe tofauti Aveva na Kaburu walikula njama za kutakatisha fedha UDS 300000.
4. Kutakatisha fedha
Aveva alijipatia fedha kutoka Barclays bank tawi la Mikocheni.
5. Kutakatisha fedha Kaburu
Kaburu alimsaidia Aveva kupata pesa USD 300,000 kutoka Barclays Bank tawi la Mikocheni.

last post see below

Next Article
« Prev Post
Previous Article
Next Post »
PEOPLE WHO COMMENT BELOW POST DROP YOUR OPINION
  • use this code to select difert type of word with bold use <strong></strong> or <b></b>.
  • for the italic use <em></em> or <i></i>.
  • To write letters underline use <u></u>.
  • To write letters strikethrought use <strike></strike>.
  • To write code HTML use <code></code> atau <pre></pre> atau <pre><code></code></pre>, And please put The code in the parser box below.

Disqus
OkUser Add your comment

Hakuna maoni