KATIKA muendelezo wa matamasha yetu ya kila mwaka, Efm redio inawaletea wasikilizaji wake tamasha la Komaa concert litakalo fanyika katika mkoa wa Mwanza na Dar es salaam, ambapo litaanza siku ya Jumamosi tarehe 8/7/2017 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kuanzia saa 4:00 Asubuhi na kufuatiwa na mkoa wa Dar es salaam tarehe 15/7/2017 katika uwanja wa Tanganyika Packers uliopo Kawe.
Tamasha hili ni la burudani pamoja na uwezeshaji, zaidi ya wasanii kumi na moja watatumbuiza katika jukwaa moja akiwemo Darasa, Rich mavoko, Ben pol, Ney wa mitego, Manfongo, Msaga sumu, chemical, na wengineo.
Vile vile katika tamasha hilo la Komaa Concert kutakuwa na mchezo wa bahati nasibu utakao chezeshwa katika mikoa yote miwili na kampuni ya BIKO ambao ndio wadhamini wakubwa wa Tamasha hili, mshindi katika mchezo huo ataondoka na zawadi ya shilingi za kitanzania milioni kumi taslimu kwa kigezo cha kuwa na elfu moja tu itakayotumika kuchezea bahati nasibu hiyo, ambapo pia tamasha litaambatana na zoezi la ugawaji wa zawadi mbalimbali kutoka kwa bwana -E kwa msikilizaji yeyote atakayekutwa anasikiliza Efm Radio.
Efm redio imekuwa ikifanya tamasha hili kwa lengo la kuwashukuru wasikilizaji wake kwa kuwa pamoja na sisi kupitia burudani pamoja na michezo itakayo wawezesha kupata fedha zitakazo wasaidia kuendeleza biashara na maisha yao kwa ujumla . Aidha kuwaonjesha wakazi wa Mwanza vionjo vya Efm redio.