Na Mwandishi wetu, Dar es salaam.
wakati Uchaguzi wa shirikisho la soka hapa Nchini TFF ukitrajia kufanyika Agosti 12 mwaka huu mkoani Dodoma imefahamika kuwa huenda Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa TFF Revocatus Kuuli akajiuzuu nafasi yake ndani ya kamati hiyo baada ya kutofautiana na wajumbe wenzake juu ya Rais anayemaliza muda wake Jamal Malinzi ambaye anashikiliwa na vyombo vya dola kwa kosa la kutakatisha fedha.
Kamati ya Uchaguzi wa TFF inajumla ya wajumbe watano ambapo kati ya hao watatu na makamu mwenyekiti Domina Madeli wanataka Jamal Malinzi apitishwe jambo linalopingwa na Kuuli.
Katika usaili wa wagombea ambao umehitimishwa leo jumamosi jumla ya wajumbe 70 wamepishishwa kati ya 72 na ilipofika wakati wa kujadili swala la Malinzi ndipo walipotofautiana.
Akizungumza mara baada ya kuvunja kikao hicho Kuuli amesema kuwa Usaili ulienda vizuri kwa wagombea wote na uamuzi wa kutumika busara kwa Jamal Malinzi umesababisha kutoelewana kwa wajumbe na kusababisha kikao hicho kuvunjika hadi kesho jumapili.
Kuuli amesema kuwa baadhi ya wajumbe wametaka busara itumike kwa wagombea ambao hawapo yaani Malinzi apitishwe hata kama hayupo na vielelezo vyake viletwe na mtu mwingine,jambo ambalo linapigwa na Kuuli.
kuuli amesema kuwa anaheshimu mawazo ya wenzake ila dhamira yake inamtuma kusimamia ukweli " Mtu hawezi kupitishwa wakati hakuwepo kwenye usaili huo na ndio msimamo wangu na leo litaendelea kujadiliwa katika kikao hiki" alisema
Tukishindwana basi mimi nitajiuzulu kuwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi TFF kwakua nina kazi nyingine za kufanya , kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Madeli amesema kuwa kwanza mwenyekiti huyi hakai Dar es salaam na maamuzi mengine yamekuwa yakifanyika bila yeye kuwepo hivyo asilipinge hili" alisema