Siku chache baada ya Mshambuliaji wa timu ya Arsenal ya Nchini England na timu ya Taifa ya Chile Alex Sanchez kutangaza kujiunga na Manchester City kwa msimu ujao Kocha mkuu wa timu ya Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa hawatamuuza mchezaji huyo kwenda Manchester City
Sanchez ambaye aliweka rekodi ya ufungaji kwa timu yake ya Taifa wiki iliyopita kwenye michuano ya kombe la Mabara ambapo leo wanatarajia kucheza na Ujeruman katika fainali ya michuano hiyo yeye alijiandaa kuondoka Arsenal lakini kocha Arsene Wenger akasema kuwa hawezi kumuuza mchezaji huyo ambaye amebakiza mwaka mmoja mataba wake umalizike na akaongeza kuwa hawatakubali ofa ya Man City bora wamtoe kwa mkopo kwenda kucheza PSG mpaka mkataba wake utakapomalizika
Ikumbukwe kuwa kabla ya msimu wa ligi kuu England kumalizika Sanchez hakuwa na furaha kikosi hapo jambo ambalo linampa kiburi kuondoka baada ya kuitumikia Arsenal misimu miwili akitokea Barcelona.