Mlinzi wa
pembeni wa timu ya taifa Shomari Kapombe huenda akaukosa mchezo wa marudiano wa
timu ya taifa ya Tanzania na Rwanda utakaochezwa julai 23 mwaka huu jijini Kigali baada ya
kuumia kifundo cha mguu wakati wa mchezo
wa taifa stars na Rwanda zikitoka sare ya kufungana bao 1-1 katika Uwanja wa
CCM Kirumba.
Kapombe
anayecheza nafasi ya mlinzi wa kushoto aliumia mnamo kipindi cha kwanza cha
mchezo huo baada ya mchezaji wa timu ya
Rwanda kuchezea vibaya hali iliyopelekea kutolewa nje na nafasi yake
kuchukuliwa na Boniface Maganga ambaye ni miongoni mwa wachezaji walioongezwa
katika timu hiyo ambaye aliimudu nafasi
hiyo mpaka mchezo mchezo ulipomalizika.
akizungumza
na Champion daktari wa timu ya taifa Richard Yomba alisema kuwa ni kweli
kapombe aliumia na kushindwa kuendelea na mchezo huo " Kapombe amepata
majeraha katika mchezo wa timu yetu na
Rwanda na akashindwa kuendelea na mchezo hivyo tunakwenda kumfanyia uchunguzi
na kwa jinsi tuivyoona anaweza kuchukua zaidi ya wiki moja kurudi katika hali
yake ya kawaida hivyo tutajitahidi kumpa
tiba apone haraka ili akaisaidie timu ya taifa" alisema
aidha Dokta
Yomba aliongeza kuwa wachezaji wengine
wa timu hiyo wako katika hali nzuri ya kuendelea na mazoezi kujiwinda na mchezo
wa marudiano " mpaka sasa ni Shomari kapombe ndiye amepata matatizo ya
kuumia kifundo cha mguu laini wengine wote wako katika hali nzuri na
tutakapoanza mazoezi jumatatu tunajua zaidi nani hayuko fiti" alisema
Chanzo: Championi.