Kaseke ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Singida United kama mchezaji huru akitokea Yanga ameliambia championi kuwa mipango ya timu hiyo ndiyo imemvutia yeye kutua Singida United " kwanza ieleweke kwamba mchezaji kuhama kutoka Yanga kwenda kokote ni jambo la kawaida lakini pia kilichonivutia zaidi ni mipango ambayo Singida wanayo kiukweli nimefurahi kujiunga na mimi pamoja na wachezaji wenzangu tutafanya vema zaidi katika ligi" alisema
aidha Kaseke ameogeza kuwa kitendo cha yeye kuungana na aliyeuwa kocha wake wa zamani wakati akiichezea Yanga kitaongeza chachu kwake kufanya vizuri zaidi " Mimi namshukuru sana Mungu kwa kunikutanisha na kocha wangu wa zamani kwani yeye ndiye alinitoa Mbeya City hivyo mimi kujiunga naye ni furaha kubwa na imani yangu n kwamba nitafanya vema katika timu kwani kocha Hans Van Der Pluijm anavitu vya ziada kabisa" alisema
Ikumbukwe kuwa Singida United tayari imefunga usajiri na inaendelea na maandalizi ya ushiriki wa ligi kuu bara ambapo timu hiyo julai 29 mwaka huu inatarajia kucheza na timu ya Lipuli fcc katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma katika mchezo wa kirafiki.