Katika hali
isiyokuwa ya kawaida wakati ligi daraja la nne ngazi ya wilaya ya Nyamagana
ikindelea mchezo baina ya Boca Junior dhidi ya Iseni fc umevunjika baada ya
wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kumshuhia kichapo mwamuzi aliyechezesha
mchezo huo Mussa Magogo eti kisa aliinyima timu hiyo penati ya wazi katika
mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Nyamagana.
Katika
mchezo huo uliovunjika mnamo dakika ya 61 ulishuhudia mashabiki wa timu ya Boca
Junior wakiruka uzio uliowekwaUwanjani hapo na kuanza kumshambulia mwamuzi huyo
hali iliyomsababishia maumivu makali na kulazimika kuvunja pambano hilo ambapo
mpaka mchezo unavunjika Iseni fc walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Alipotafutwa
Mwamuzi Mussa Magogo kuzungumzia kipigo alichopata alikiri kupigwa na mashabiki
hao na kumsababishia maumivu makali " ni kweli nimepigwa na hiyo hali
ilitokea wakati mchezo unaendelea ambapo shabiki wa Boca Junior aliruka ukuta
na kunifuata Uwanjani na kuanza kunipiga pamoja na baadhi ya wachezaji na
nimepata maumivu makali ila namshukuru Mungu kwa sasa naendelea vizuri"
alisema.
Naye
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya chama cha soka wilaya ya Nyamagana
NDFA Suleiman Kiggi amesema kuwa soka
bila nidhamu haliwezi kwenda mbele " Sisi kama NDFA tunalaani kitendo
walichokifanya Boca junior kwa kumpiga Mwamuzi wetu na tutahakikisha kuwa
tunatoa adhabu stahiki kwa timu hiyo ili iwe funzo kwa wengine na tunasubiri
ripoti ya waamuzi na msimamizi wa mchezo (kamisaa) ili tuweze kutoa maamuzi hivyo
lazima timu ziwe na nidhamu ziwapo Uwanjani" alisema