Aliyekuwa Mwamuzi mstaafu wa Ligi kuu bara na
kamisaa wa shirikisho la Soka hapa nchini TFF Omary Juma amefariki dunia baada
ya kulazwa katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure baada ya kuugua ghafla.
Mwenyekiti wa Chama cha waamuzi Mkoa wa Mwanza
Emmanuel Mataba amesema kuwa wamepoteza mtu muhimu ambaye pengo lake haliwezi
kuzibika " kimsingi taarifa za msiba za mzee wetu kwani alikua mzee ambaye
alikua akitushauri katika jinsi ya kuendesha Chama hivyo Kazi ya mungu haina
makosa" alisema
Tayri marehemu Omary Juma amezikwa katika makaburi ya Nyakato yaliyoko wilayani Ilemela jijini hapa.
Ikumbukwe kuwa mpaka umauti unamkuta mzee Omary Juma
alikua kamisaa wa shirikisho la Soka hapa nchini TFF ambapo alikua akisimamia
baadhi ya mechi za Ligi kuu bara na Ligi daraja la kwanza.