Siku chache baada ya shirikisho la Soka hapa nchini
TFF kutangaza makundi matatu yatakayoshiriki Ligi daraja la kwanza msimu ujao
Uongozi wa timu ya Pamba ya jijini hapa umeiijia juu Bodi ya Ligi ambao
ndio wapangaji wakuu wa ratiba kwakuziweka timu za Mwanza katika kundi moja.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Bob Butambala
amesema kuwa inashangaza kuona timu zote za mwanza zinawekwa katika kundi moja
" Mwanza tulikua na mkakati wa kupandisha timu zaidi ya moja lakini
kitendo cha bodi ya ligi kutuweka kundi moja kimetuvunja moyo na hatujui sababu
ya kupangiwa hivyo" alisema
Aidha Butambala alisema kuwa kitu ambacho
kingefanyika ilitakiwa timu hizo zipangwe makundi tofauti ili kila timu
ipambane kivyake" kitendo cha kutuweka sisi Pamba, Toto na Alliance katika
kundi moja ni kudumaza Soka kwani Mkoa wa mwanza unahitaji kuwa na timu zaidi
ya moja hivyo tunaomba bodi ya Ligi waliangalie hili" alisema
Ikumbukwe kuwa Pamba FC iko katika kundi C ambalo
lina timu za Toto African, Alliance, Polisi Mara, Jkt Oljoro, Rinho Rangers,
Transtcamp pamoja na Polisi Dodoma amnapo kwa msimu huu ligi daraja la
kwanza inajumla ya makundi matatu.