NEYMAR ATIMKA BARCELONA

Julai 28, 2017
Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania Mrazil  Neymar Dos Santos leo ametawala upya vichwa vya habari  baada ya kuvua jezi ya mazoezi ya Barcelona na kuondoka uwanjani baada ya kugombana na mchezaji mwenzake Nelson Semedo wakiwa mazoezini.
Neymar alikuwa mazoezini na katika hali isiyokuwa ya  kawaida kulitokea kutokuelewana kati yake na mchezaji mpya wa klabu hiyo Nelson Semedo ndipo Neymar alipokasirika na kuanza kuzichapa.
Neymar alionekana kutaka kumkabili Semedo lakini wakati anamfuata huku akionekana mwenye hasira ndipo Sergio Bosquet na Javier Mascherano walimzuia.
Baada ya Neymar kuzuiwa kuendeleza ugomvi alivua jezi maalumu ya mazoezi (bibs) akaitupa pembeni kisha akaupiga mpira kwa hasira na kuondoka zake.
Neymar amefanya tukio hilo katika kipindi hiki ambacho anahusishwa na uhamisho wa kwenda katika klabu ya PSG na huku ikitajwa kwamba hana furaha na Barcelona.
Tukio hili limezidi kuongeza tetesi kwamba Neymar anaweza kuondoka Barca lakini Barca kwa upande wao pia wamechoshwa  na tabia za Neymar haswa starehe zake.

last post see below

Next Article
« Prev Post
Previous Article
Next Post »
PEOPLE WHO COMMENT BELOW POST DROP YOUR OPINION
  • use this code to select difert type of word with bold use <strong></strong> or <b></b>.
  • for the italic use <em></em> or <i></i>.
  • To write letters underline use <u></u>.
  • To write letters strikethrought use <strike></strike>.
  • To write code HTML use <code></code> atau <pre></pre> atau <pre><code></code></pre>, And please put The code in the parser box below.

Disqus
OkUser Add your comment

Hakuna maoni