Katika
kuhakikisha kuwa timu za Mwanza zinafanya vema katika mashindano yanayozikabili
Chama cha soka wilaya ya Nyamagana NDFA kimeandaa ligi ndogo ambayo
itazikutanisha timu za Alliance, Pamba, Toto african pamoja na Mbao katika
kujiandaa kuelekea ligi daraja la kwanza na ligi kuu bara.
Akizungumza
na mtandao huu Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya chama hicho Suleiman Kiggi
amesema kuwa wao kama Chama wameamua kuunda ligi hiyo ambayo itazisaidia timu
hizi kujua mapungufu yao " hapa Mwanza tunazo timu nne ambazo zinatarajiwa
kushiriki michuano ya ligi kuu na ile ya ligi daraja la kwanza hivyo sisi
tumeamua kuanzansiaha ligi hii ili timu hizo zikutane na ziweze kubaini
mapungufu ili yafanyiwe kazi kaba ya ligi kuanza" alisema
aidha Kiggi
amesisitiza kuwa mpaka sasa timu ambayo imethibitisha kushiriki katika ligi
hiyoo ni Pamba fc " baada ya kuunda ligi ikabidi tutye barua kwa timu
huzika ili ziridhie na mpaka sasa Pamba peke yao ndio wamethibitisha kushiriki
hivyo tunaziomba timu zingine zithibitishe ushiriki ili maandalizi yafanyike
mapema kwani tunampango mzuri na timu zetu" alisema
Kiggi
amebainisha kuwa michuano hiyo inatarajia kuwanza kurindima kuanzia agosti 6
mpaka agosti 10 hivyo kila timu itakutana na timu nyenzake " mashindano
yetu tumepanga yafanyike kwa siku nne ili timu zijaribu wachezaji wake ili kama
ni kufanya mabadiriki yafanywe mapema na tunaamini ligi hii itazisaidia timu
zetu kuleta ushindani kwenye ligi kuu na ligi daraja la kwanza na tumejipanga
kufanya hivyo kila mwaka" alisema.