Na Johnson
James, Mwanza
Pamba fc ya
jijini hapa inayojiandaa kushiriki ligi
daraja la kwanza msimu ujao imeendeea na maandalizi yake kwaajili ya msimu ujao
ambapo imefanikiwa kuichapa timu ya Buseresere fc kwa jumla ya bao 2- katika
mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa
Katoro stadium uliopo mkoani Geita.
Katika
mchezo huo ambao ulikuwa maalumu kwa kuchuja wachezaji ambao wataitumikia Pamba
fc katika ligi daraja la kwanza msimu ujao ulishuhudia timu ya soka ya Pamba
ikionyesha kandanda safi ambapo mabao ya washindi walifungwa na Miraji Salehe
dakika ya 28 pamoja na Shaban Binamungu aliyefunga bao dakika ya 88 ya mchezo
huo na kupelekea Buseresere fc kulala kwa bao 2-0.
Mara baada
ya mchezo huo Kocha wa Pamba fc Mathias Wandiba amesema kuwa lengo la kucheza
mchezo huo wa kirafiki ni moja ya maandalizi ya Pamba kuelekea ligi daraja la
kwanza msimu ujao " Kimsingi sisi kama Pamba tayari tumeanza maandalizi
yetu na kwa sasa tunaendelea kuimarisha kikosi chetu lengo la kuanza mapema ni
kuhakikisha kuwa Pamba inapanda kuchezaligi kuu bara msimu ujao kwani tumejipanga kufanya vizuri zaidi"
alisema
aidha
Wandiba ameongea kuwa akiwa mkoani Geita atacheza michezo mingi ya kirafiki
lengo ni kukiweka sawa kikosi chake " nitahakikisha kuwa nacheza michezo
mingi ya kirafiki ambapo malengo ya kufanya hivyo ni kuwajengea uwezo wachezaji
wangu wa kucheza muda mrefu bila kuchoka lakini pia kuwa na uwezo wa kuhimili
changamoto za ligi daraja la kwanza kwani ukiwanda wachezaji mapema kiukweli
lazima timu ifanye vema katika ligi" alisema