Na Mwandishi wetu, Pritoria
Kiungo wa timu ya Simba Muzamiru Yasin yuko nchini Afrika Kusini akiitumikia timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) katika michuano ya Cosafa ambayo imetinga nusu fainali kwa kuwatoa wenyeji Afrika Kusini bao 1-0 na kutinga hatua ya nusu fainali.
Taarifa zinaeleza, mawakala kadhaa wameanza kumfuatilia kwa karibu baada ya kuwa mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri zaidi katika michuano ambapo mpaka sasa mchezaji huyo amekuwa mchezaji bora katika moja ya mechi alizocheza.
Baadhi ya magazeti ya Afrika Kusini yameeleza kuwa nyota huyo wa Simba na timu ya taifa amekuwa lulu kutokana na uwezo aliyo uonyesha katika mechi zote ambazo Stars imechezana kupata matokeo.
Imeelezwa miongoni mwa timu zilizovutiwa ni Bidvest na Mpumalanga Black Ace lakini wataalamu wanaofuatilia wachezaji(mawakala) wanaweza kuwapeleka wachezaji hata katika timu za nje ya Afrika Kusini.
Katika michuano hiyo Muzamiru amekuwa injini kuu ya kuendesha kiungo cha Stars na kusababisha mvuto mkubwa kwa watazamaji ambapo Stars katika michezo minne tuliyocheza tumeshinda michezo miwili na kutoa sare mchezo mmoja Na kama mambo yakiendelea vizuri mzamilu anaweza kusepa zake nje ya nchi kucheza soka la kulipwa..