Uongozi wa bia ya Serengeti Primier Lager ambao ndio wadhamini wa kuu wa timu ya taifa ya Tanzania umesema kuwa watahakikisha kuwa wanaongeza hamasa kwa watanzania ili waendelee kuipenda timu yao zaidi.
Akizunumza na Mtandao huu Ofisa mawasiliano wa bia hiyo John Wanyacha amesema kuwa wamejioanga kuhakikisha kuwa timu hiyo inaimarika siku hadi siku " kimsingi tangu tumerudi kuidhamini timu ya taifa tumeona maendeleo makubwa hivyo tumejipanga kuwahamasisha watanzania kuipenda timu yao ya taifa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma" alisema
Ikumbukwe kuwa wikendi iliyopita timu ya taifa ilicheza na timu ya taifa ya Rwanda na kutoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.