Na Mwandishi wetu,
Timu ya soka ya Singida United imeichapa timu ya Pamba kwa jumla ya bao 5-0 katika mchezo maalumu wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Nyamagana jijini hapa mchezo huo ulikuwa maalumu kwa timu ya Pamba kuchuja wachezaji itakaowatumia katika msimu ujao wa ligi daraja la kwanza.