Na Mwandishi wetu, Mwanza
Timu ya soka ya Singida United ya mkoani Singida imeichapa timu ya Alliance sports academy inayojiandaa na ligi daraja la kwanza msimu ujao kwa jumla ya bao 2-0 katika mchezo wa kirafiki uiopigwa Uwanja wa Nyamagana jijini hapa , katika mchezo huo uliokuwa wa ushindani wa aina yake ulishuhudia Aliance sports academy wakishindwa kutumia nafasi walizopata baada ya mlinda mlango wa Singida United Said Lubawa kupangua mikwaju miwili ya penati waliyopata Alliance
Mabao ya Singida United yalifungwa na Elisha Muroiwa pamoja na TwafadzwaKutinyu aliyefunga bao kwa mkwaju wa penati.