Na Mwandishi wetu, Mwanza
TAASISI ya kuzui na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mwanza
inawashikilia
wagombea wanne wa TFF pamoja na wajumbe wapiga kura sita kwa viashiria vya
utoaji na upokeaji Rushwa kuelekea
uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka hapa nchini TFF unaotarajia kufanyika agost
12 mkoani Dodoma..
Akizungumza na mtandao huu mkuu wa Taasisi hiyo mkoani hapa Erenest Makale amekiri kuwa viongozi hao wanashikiliwa na tasisi yake toka jana usiku baada ya wasamalia wema kutoa taarifa ya hali waliyokuwemo pamoja na mazingira yake.
"Unajua kwa sasa zimebaki wiki mbili tu uchaguzi wa TFF ufanyike na hii inaonyesha kuwa ni dalili ya kuwa ni viashiria vya utoaji wa Rushwa mara baada ya kuonekana mazingira yote yalikuwa wazi lakini pia tunaendelea na uchunguzi,"alisema.
Makale pia alisema kuwa watuhumiwa hao walipohojiwa walisema kuwa walionekana wazi kuwa wanatumia genge la uzinduzi wa michuano ya Sports Extra ndondo Cup kufanikisha azima yao, na kama wasimamizi tumeamua kutoa tamko la kuzuia kitu kinachoitwa ndondo hadi uchaguzi upite.
"Na kwenye hili inasemekana walikuwa wazindue Mwanza na badae Mbeya lakini pia wangerudi Mwanza hivyo tumeamua itulie kwanza kupisha uchaguzi, na baada ya kuzungumza nao maelezo yao yalijichanyanga na ilionekana wazi kuwa walitumia hii fursa kufanya wanayotaka ila lazima watambue kuwa Mkono wa serikali ni mrefu mno hivyo wengine wakaochonjo " alisema Makale.
Makale pia aliwataja viongozi walioshikiliwa kuwa ni Shaffih Dauda, Elias Mwanjale, Benester Lugola, Almasi Kosongo, Leonard Malongo, Epharahimu Majinge Osuli Kosuli, Richard Kayenzi, Kelvin Shevi na Lazark Juma.
Makale pia amewataka wagombea wote kuelekea uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka hapa nchini TFF kuwa makini na kutojihusisha na vitendo vya Rushwa ili wawe na chachu ya kuwatendea haki wananchi waliowachagua.
Aidha kuzuia taratibu za ndondo cup kuendelea jijini hapa zimekuja muda mchache baada ya kufanyika uzinduzi huo uliofanyik villa park Resort iliyopo wilayani Ilemela jijini hapa..
tayari watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana na uchunguzi
unaendelea.