Yale mashindano ya Sports Extra Ndondo cup ambayo hufanyika jijini Dar es salaam kwa mwaka wa nne mfululizo , yamezinduliwa jijini Mwanza ambapo mashindano hayo kwa mara ya Kwanza yatachezwa jijini hapa ambapo yataanza kutimua vumbi rasmi septemba 9 mwaka huu na kusimamiwa na Chama cha soka mkoa wa Mwanza.
Katika Uzinduzi huo uliohudhuriwa na Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza James Bwire waandaaji wa michuano hiyo Clouds media kupitia kipindi chao cha Sports Exra kupitia kwa mwakili wao Yahya Mohamed amesema kuwa lengo la kuleta mashindano hayo jijini Mwanza ni kuhakikisha kuwa vipaji vya soka vinakuzwa ipasavyo lakini pia timu zitakazoshiriki michuano hiyo zitakuwa 16 na utaratibu wa kushiriki ni kuwahi kujiandikisha na sio vinginevyo, Mohamed zmeziomba timu kuwa na ubunifu ili michuano hiyo iwe na faida katika soka la Mwanza.